
STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 26.06.2018

RAIS wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za
pongezi Rais wa Msumbuji, Felipe Nyusi kwa kutimiza miaka 43 tokea kupata Uhuru
kwa Taifa hilo.
Salamu hizo zilieleza kuwa kwa niaba yake Dk.
Shein, wananchi pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanaungana pamoja
na ndugu zao wa Msumbuji katika kusherehekea siku hiyo adhimu ya uhuru wa Taifa
hilo.
Aidha, katika salamu hizo, Dk. Shein
alimuhakikishia Rais Nyusi kuwa Zanzibar itaendeleza uhusiano na ushirikiano
mkubwa uliopo kati yake na nchi hiyo sambamba na kuimarisha udugu uliopo kati
ya wananchi wa pande mbili hizo.
Pia, salamu hizo zilieleza namna ya Zanzibar
itakavyoimarisha ushirikiano uliopo kati yake na Msumbuji kwa kukuza uhusiano
mwema wa kikanda na kimataifa.
Pamoja na hayo, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kumtakia
Rais Nyusi afya njema yeye na familia yake na kumtakia maisha marefu yenye
furaha pamoja na sherehe njema ya siku hiyo adhimu ya uhuru wa Taifa hilo kwa
amani, utulivu na upendo kwa maendeleo endelevu ya wananchi wa Msumbiji.
Msumbiji ilipata uhuru wake Juni 25 mwaka 1975
kutoka kwa koloni la Wareno chini ya Jamedari wake Samora Machel ambaye hatimae
ndiye aliekuwa Rais wa kwanza wa Msumbuji huru.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment