Habari za Punde

Uhakiki wa Wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF Kuaza Kuhakikiwa Mwazoni Mwa Mwezi Julai 2018.


MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR (ZSSF) UNAWATANGAZIA WASTAAFU WANAOPOKELEA PENCHENI YA ZSSF KUPITIA BENKI TOFAUTI KUWA UHAKIKI KWA WANACHAMA SASA UTAFANYIKA MWANZONI MWA MWEZI WA JULAI 2018
KWA WASTAAFU WOTE WA UNGUJA NA PEMBA UHAKIKI HUO UTAFANYIKA KUANZIA TAREHE 01 HADI 08 JULAI 2018 KUANZIA SAA 2:00 ZA ASUBUHI 
UHAKIKI HUO UTAFANYIKA KATIKA AFISI ZA ZSSF KILIMANI MNARA WA MBAO NA TIBIRINZI CHAKECHAKE PEMBA.

AIDHA KWA WASTAAFU WALIOPO DAR ES SALAAM UHAKIKI WAO UTAFANYIKA KUANZIA 02/07/2018 HADI 05/07/2018 KATIKA AFISI ZA URATIBU WA SHUGHULI ZA SMZ ZILIZOPO MTAA WA OHIO KARIBU NA MAKAO MAKUU YA BENKI KUU YA TANZANIA - BOT

INASISITIZWA KUWA UHAKIKI HUO NI KWA SIKU SABA TU. WASTAAFU WATAKAPOKWENDA KUHAKIKIWA WANATAKIWA KUCHUKUA VITAMBULISHO VYAO VYA ZSSF NA ASIYEHAKIKIWA PENCHENI YAKE ITAZUIWA.
AIDHA ZSSF INAWATANGAZIA WANACHAMA WAKE KUWA KWA SIKU HIZO ZA UHAKIKI (YAANI 01 – 08 JULAI 2018) HUDUMA ZA USAJILI WA WANACHAMA PAMOJA NA MAFAO ZITASIMAMA HADI KUMALIZIKA KWA ZOEZI LA UHAKIKI.
KILA ATAKAESIKIA TANGAZO HILI AMUARIFU MWENZIWE.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.