Habari za Punde

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar.Mhe. Khalid Salum Mohammed Akiwasili Katika Viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Kuwasilisha Hutuba ya Bajeti ya Serikali leo.

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed akiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar, akionesha Brifcase yenye Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akionesha kwa Waandishi wa Habari walioko katika viwanja vya Baraza kuripoti. 
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed akifurahia jambo wakati akiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Zanzibar akionesha Mkoba wa Matumizi na Mapato ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa waandishi wa Habari Zanzibar.

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed akishindikizwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati akiingia katika ukumbi wa Mkutano wa Kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar kuwasilisha Hutuba ya Bajeti ya Matumizi na Mapato kwa wa Fedha 2018/2019. 
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakishangilia wakati Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed akiingia katika ukumbi wa Mkutano wa Kumi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi kuwasilisha Hutuba ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Wajumbe leo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.