Habari za Punde

Foleni Mji Mkongwe kero kwa Wakaazi

Kreni kubwa ambalo limeanza kufanya kazi kulikarabati jengo la Beit Al Ajaib likionekana kwenye picha na kusababisha msururu wa foleni ya magari katika eneo la mji mkongwe leo.
Hii ni sehemu ya foleni kubwa iliyosababishwa na kuanza kwa ujenzi na ukarabati wa jengo la Beit Al Ajaib katika mji mkongwe.


Na Mkaazi wa mji Mkongwe
Kuna maamuzi yanafanyika unashangaa nini malengo yake mbali na kuwaongezea kadhia wakaazi wa Mji Mkongwe? Hii ndio busara inayotawala.

Njia zote zilizokuwa zikitumika Mji Mkongwe zimefungwa (sasa zote ni njia moja - one way) wakati barabara iliyopo ni nyembamba, kuna matengenezo kibao, kuna Gati, kuna Forodhani, kuna wageni, na kuna soko la samaki. 

Safari ya dakika tano sasa inaweza kukuchukua masaa mawili. 

Sasa ujenzi Jumba la Ajabu umeanza. Leo kuna hilo crane linabanjua sehemu ya Varanda. Likiwa kazini gari zote zimesimamishwa. 

Wakaazi wa Mji Mkongwe tuendelee tu na hali hii ya kupotezewa muda katika foleni zinazoepukika? 

Utendaji na maamuzi ya aina haya yana tija gani kwa wakaazi na watumiaji wa barabara?

baraza la Manispaa halikuwa na mpango maalum wa kushughulikia tatizo hili la foleni wakati wanajua kwamba ujenzi wa Jengo la Ajabu unaanza?


Kama unakaa maeneo ya Shangani, Forodhani, Kiponda, Malindi...huepukani na hali hii kwa vile lazima uzunguke Malindi utadima tu katika foleni na haitabiriki wakati gani njia utakuwa afadhali. 

Omba usikutane na meli za Dar na Pemba pia hali huwa mbaya zaidi.

Chondechonde jamani na sisi wakaazi wa mji Mongwe tunastahiki kuangaliwa tuna haki zetu kama wakaazi wa mji mkongwe, Jamani busara itumike.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.