Habari za Punde

Mkurugenzi wa Uchaguzi Tanzania Mhe. Dkt. Athumani Kihamia Akagua Maandalizi ya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani Manispa ya Moshi Arusha na Longido.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (katikati) akipokea taarifa ya maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 4 za jimbo la Arusha kutoka kwa Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo Namyaki Wilfred Laitetei.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (katikati) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Halmashauri ya wilaya ya Longido kufuatilia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 4 . Kushoto ni Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Longido Bw. Jummaa Mohamed Mhina na Kulia ni Afisa kutoka NEC, Bw. Athuman Masesa.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (katikati) akizungumza jambo na Msimamizi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Moshi Bw. Michael Mwandezi (kulia) mara baada ya kuwasili katika Manispaa hiyo kufuatilia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 1 . Kushoto ni Afisa kutoka NEC, Bw. Athuman Masesa.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Moshi Bw. Michael Mwandezi (kulia) akimweleza jambo Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (katikati) mara baada ya mkurugenzi huyo kuwasili katika Manispaa ya Moshi kufuatilia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 1 Agosti 12 mwaka huu . Kushoto ni Afisa kutoka NEC, Bw. Athuman Masesa.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (kulia) akipokea taarifa ya maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 4 za jimbo la Longido kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Longido Bw. Jummaa Mohamed Mhina.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Msimamizi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Moshi Bw. Michael Mwandezi (wa pili kutoka kulia) na Maafisa wa Uchaguzi jana mjini Moshi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.