Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akiagana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ndg. Balandya Mayuganya Elikana (kulia) mara baada ya Jaji Mwambegele kumtembea na kufanya mazungumzo ofisi kwake Mkoani Mwanza leo Julai 03, 2025. Jaji Mwambegele yupo mkoani Mwanza kukagua mwenendo wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaoendelea katika Magereza ya Tanzania Bara na Vyuo vya mafunzo kwa Zanzibar katika zoezi lililoanza Juni 28 na litamalizika Julai 04,2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akisalimiana na Mkuu wa Gerreza Kuu la Bitimba Mkoani Mwanza ACP. Pascal Temba na Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza, SACP. Masoud Kimolo. Jaji Mwambegele alitembelea gereza hilo leo Julai 03, 2025 katika mwendelezo wa ziara zake za kukagua mwenendo wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaoendelea katika Magereza ya Tanzania Bara na Vyuo vya mafunzo kwa Zanzibar katika zoezi lililoanza Juni 28 na litamalizika Julai 04,2025. (Picha na INEC).
No comments:
Post a Comment