WACHEZAJI wa Ngombe wakimpiga ngea (Chenga) ng'ombe, wakati wa tamasha la Utalii, Utamaduni na Bishara lilifanyika katika uwanja wa Dodo Pujini Wilaya ya Chake Chake Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WACHEZAJI wa Ngombe wakimpiga ngea (Chenga) ng'ombe, wakati wa tamasha la Utalii, Utamaduni na Bishara lilifanyika katika uwanja wa Dodo Pujini Wilaya ya Chake Chake Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
NA ABDI
SULEIMAN, PEMBA
NG’OMBE
mwenye jina la Toba Roho yangu na Kiburungo, ambao hupendwa kuchezwa katika
mchezo wa Ng’ombe, ameendelea kuwavutia hisia za mashabiki wa mchezo huo
Kisiwani Pemba.
Ng’ombe wengine ambao wameweza kutumika katika
mchezo huo ni pamoja na Baruti na Ubamba, ambao ni Ng’ombe wapya kuingia katika
mchezo huo.
Ngombe hao wamekuwa maarufu katika mchezo huo,
ambapo mchezo huo umefanyika katika viwanja vya Pujini ikiwa ni kuelekea kilele
cha Tamasha la Utalii, Utamaduni na Biashara Pemba, lililo chini ya Kamisheni
ya Utalii Zanzibar.
Mchezo huo umeweza kushuhudiwa na wananchi kutoka
maeneo mbali mbali ya Kisiwa Cha Pemba, wakiwemo Mji wa Chake Chake na maeneo
jirani.
Mchezo huo ulioanza saa 11:00 jioni huku mashabiki
wengi wakijitokeza katika mchezo huo, akizungumza mara baada ya kumaliza kwa
mchezo huo Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, alisema mchezo
wa ng’ombe ni Utamaduni Pekee wa nanchi wa Kisiwa Cha Pemba.
Alisema serikali yake ya Mkoa itahakikisha
inashirikiana kikamilifu wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale, katika
kuhakikisha michezo yote ya utamaduni iliyokuwa ikifanyika inafufuliwa upya na
kuchezwa katika vipindi vyote na sio kwenye matamasha pekee.
“Mchezo huu unaonekana unapendwa sana leo hebu
angalieni watu waliojitokeza, vizuri tukafufua michezo yetu yote ya asili
tuliokuwa tukiicheza”alisema.
Alisema kufanyika kwa michezo hiyo itaweza kuvutia
watalii kupenda kutembelea kisiwa cha Pemba, pale itakapokuwa na vipindi
maalumu na kuweza kukitangaza kisiwa cha Pemba ndani na nje ya nchi zao.
Mkuu huyo alisema kuongezeka kwa watalii wataweza
kuongeza pato la nchini, hata uchumi wa Zanzibar nao pia utaweza kuongezeka na
vijana kupata ajira kupitia sekta hiyo.
Kwa upande wao wachezaji wa Ng’ombe Kisiwani Pemba,
wamesema tayari mchezo huo umeshaanza kupoteza uhalisia wake kutokana na
kutokufanyika mara kwa mara.
Walisema mchezo huo hapo awali ulikuwa
ukifanyika katika maeneo mbali mbali, hasa baada ya mavuno muda wa jioni kwa
lengo la kupongezana, hivyo ipo haja kwa taasisi husika kujipanga kikamilifu
kuurudisha utamaduni wa mchezo huo wa asili ya kisiwa cha Pemba.
No comments:
Post a Comment