MSAFARA wa Punda 15 wakiwa katika Gawaride maalumu la Punda, kutoka Chanjaani hadi Pujini wakati wa Tamasha la Utalii, Utamaduni na Biashara lililofanyika Pujini
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
NA ABDI
SULEIMAN, PEMBA
KWA mara ya
kwanza wananchi wa Kisiwa Cha Pemba wameshuhudiwa Gwaride lan Punda, lilianzia
Chanjaani hadi Pujini Wilaya ya Chake Chake.
Gwaride hilo lilianza saa nane za mchana katika
uwanja wa Zimamoto Chanjaani, kupitia barabara ya Pujini hadi katiak uwanja wa
dodo Punji, huku punda wakiwa wamefolini mistari na waendeshaji wake wakiwa
wamevaa kanzu na miemvuli.
Baada ya kufika katika uwanja wa Pujini, punda hao
waliweza kukimbia raundi mbili kwa kuzunguruka kila mmoja kuonyesha umahiri
wake katika kwenda mbio.
Gwaride hilo lilijumuisha jumla ya Punda 15 kutoka
maeneo ya Matale na Pujini, huku baadhi yao wakiongozwa na watoto wadongo na
watu wazima.
Gwaride hilo maalumu na mara ya kwanza katika Kisiwa
Cha Pemba, limeweza kuvuta hisia za wananchi wengine kujikuta wanashangiria
kutokana na aina ya uchezaji wake.
Baadhi ya wananchi waliokuwa wakishuhudiwa
walisikika wakisema kuwa, hili ni jambo la faraja kufanyika kwa gwaride hilo,
kwani wamezoea kuona mashindano ya farasi tu.
Walisema kama mchezo huo utakuwa unafanyika kila
kipindi, basi punda watakuwa na thamani kuliko walivyozoeleka tu kutumika kwa
kupakia mizigo.
Saidi Khamis Omar mwenye umri wa miaka 14 mkaazi wa Matale, alisema ni mara ya kwanza kwake kucheza gwaride la Punda, huku akiwaomba
waandaaji kuendelea kufanyika maonyesho hayo mara kwa mara, ili kuweza kupata
nafasi ya kujitangaza na kuutangaza mchezo huo.
Khamis Omar Khamis alisema kwake amezoea kuona
mchezo wa ngombe na mashindano ya farasi, kushiriki katika gwaride hilo la Punda
ni mara ya kwanza katika maisha yake.
“Tokea kuzaliwa kwaku sijawahi kushiriki hata mara
moja, hii kwangu ndio mara ya kwanza, tumekua tukiona mashindano yam bio za
Farasi kumbe na punda nao wanaweza pale wakiwezeshwa waendeshaji wake”alisema.
Alisema pindi mchezo huo kama utaendelezwa basi
utaweza kuvuta mashabiki wengi, hata wataalii kutoka maeneo mbali mbali kufika
kujionea, kitu ambacho kitakitangaza Kisiwa Cha Pemba.
Salum Haji Khamis aliiomba Wizara ya Habari Utalii
na
Mambo ya Kale, kuuendeleza mchezo huo nao kuweza kuchezwa kila kipidni cha
matamasha kama ilivyo mchezo wa ng’ombe.
No comments:
Post a Comment