Habari za Punde

Onesho la Usiku wa Sanaa Kisiwani Pemba Wafana.

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Amour Hamili Bakari, akizungumza wakati wa usiku wa sanaa, ikiwa ni ufungaji wa tamasha la 23 la Utamaduni wa Mzanzibari, lilofanyika katika viwanja vya Gombani Chake Chake Pemba.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akitoa salamu za wananchi wa Mkoa wa Kusini na Kaskazini, wakati wa usiku wa sanaa ikiwa ni Ufungaji wa Tamasha la 23 la Utamaduni wa Mzanzibari, lililofanyika katika viwanja vya michezo Gombani
BAADHI ya Wafanyakazi wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba, wakifuatilia kwa makini Tamasha la 23 la Utamadunia wa mzanzibar, katika usiku wa sanaa uliofanyika katika viwanja vya Gombani Nje
MSANII Salum Abdalla (Kachara) akisoma risala ya wasanii wa Kisiwa cha Pemba, wakati wa ufungaji wa Tamasha la 23 la Utamaduni wa Mzanzibar, katika usiku wa sanaa huko katika viwanja vya Gombani Chake Chake
VIONGOZI mbali mbali wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar, wakiongozwa na Naibu waziri wa Wizara hiyo Lulu Msham Abdalla, kushoto ni Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo Amour Hamil Bakari na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, wakifuatilia kwa makini Usiku wa Sanaa uliofanyika katika viwanja vya Gombani, ikiwa ni ufungaji wa Tamasha la 23 la Utamaduni wa mzanzibari
NAIBU waziri wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Lulu Msham Abdalla, akisalimiana na Salum Abdalla(Kachara) mara baada ya kumaliza kusoma risala ya wasanii wa Kisiwa Cha Pemba wakati wa usiku wa sanaa, ikiwa ni Ufungaji wa Tamasha la 23 la Utamaduni wa mzanzibari
NAIBU wa Wizari wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar, Lulu Msham Abdalla akisoma taarifa ya Ufungaji wa Tamasha la 23 la Utamaduni wa Mzanzibari lilioambana na Usiku wa sanaa, huko katika viwanja vya uwanja wa michezo Gombani
WASANII wa Kikundi cha Maigizo cha Mwinyi Mpeku Kutoka Wete, wakiimba Wimbo maalumu wa Mohamed Kombo (Mwinyi Mpeku Peku la Ungo) wakati wa Usiku wa Sanaa, katika kilele cha Tamasha la 23 la Utamaduni wa Mzanzibari, lililofanyika katika Viwanja vya Gombani Chake Chake Pemba
VIJANA Warhad Mohammed na Ulfat Juma akisoma utenzi maalumu wa Tamasha la 23 la Utamaduni wa Mzanzibari, katika usiku wa sanaa ikiwa ni ufungaji wa tamasha hilo, lililofanyika katika viwanja vya michezo Gombani
WASANII wa Kikundi cha Sanaa cha Ngoma ya Msewe Kisiwani Pemba, wakiingia katika usiku sanaa ikiwa ni kilele cha Tamasha la 23 la Utamaduni wa Mzanzibari, huko katika viwanja vya GombaniChake Chake Pemba
WASANII wa Kikundi cha Sanaa cha Mwinyi Mpeku Kutoka Wete, wakiongozwa na Salum Abdalla Kachara kushoto na Mohammed Kombo Mwinyi Mpeku Peku la Ungo Kushoto, wakiwa na wasanii wenzao Kitatange wakitoa maoja ya igizo katika usiku wa sanaa, ikiw ani ufungaji wa Tamasha la 23 la Utamaduni wa Mzanzibari lililofanyika viwanja vya Gombani
WASANII wa Kikundi cha Maigizo cha Mwinyi Mpeku Kutoka Wete, wakiimba Wimbo maalumu wa Mohamed Kombo (Mwinyi Mpeku Peku la Ungo) wakati wa Usiku wa Sanaa, katika kilele cha Tamasha la 23 la Utamaduni wa Mzanzibari, lililofanyika katika Viwanja vya Gombani Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman - Pemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.