Habari za Punde

Uzinduzi wa Tamasha la 21 la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF Viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar. Maulid ya Home Yafanisha ZIFF Jana Usiku.

Uzinduzi wa Tamasha la 21 la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF lazinduliwa kwa kupandisha Tanga kuashiria Jahazi linaaza safari yake katika Viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar, Tamasha hilo limezinduliwa jana usiku na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu.
WAJUMBE wa Bodi ya ZIFF Zanzibar wakishuhudia Uzinduzi wa Tamasha la 21 la Nchi za Jahazi Zanzibar, lililofanyika katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar , wakati likipandishwa Tanga kuashiria Uzinduzi huo
Mkurugenzi Mtendaji wa ZIFF Zanzibar Daniel Nyalusi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 21 la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF, kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo. kuzungumza na kumkaribisha Mgeni Rasmin Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa ZIFF Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Tamasha la 21 la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF, katika ukumbi wa Ngome Kongwe Zanzibar. 
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF Zanzibar. Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiwatambulisha Wajumbe wa Bodi ya Ziff wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 21 la Nchi za Jahazi Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya ngome kongwe Zanzibar

Muigizaji na Producer wa Filmau kutoka Nchini Nigeria Bi. Bikiya Graham, akiwasalimia Wananchi wa Zanzibar wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la 21 la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar
Actor na Director wa Filmau kutoka Nchini Burkina Faso Ndg. Jacky Ido, akiwasalimia Wananchi wa Zanzibar wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la 21 la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Issa Haji Gavu  akiwa na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo wakifuatilia ufunguzi wa Tamasha hilo katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.