Habari za Punde

ANZISHENI KAMATI ZA MAZINGIRA KATIKA NGAZI ZOTE - MAKAMBA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na mamia ya wakazi wa Mkoa wa Tabora (hawapo pichani) waliojitokeza katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kumsikiliza. Waziri Makamba amezindua Kamati ya Mazingira na kuwataka wananchi hao kuwa mstari wa mbele kusimamia masuala ya mazingira katika maeneo yao


Jamii imetakiwa kufahamu kuwa Kamati za Mazingira katika 

ngazi zote zipo kwa mujibu wa Sheria, Sheria ya Mazingira 

kifungu Na. 38 (1-2) na Kamati hizo zina wajibu wa 

kusimamia mazingira kikamilifu yanayohusu maeneo yao.

Akizungumza na Watendaji wa Mkoa wa Tabora katika hafla 

ya kuzindua Kamati ya Usimamizi wa mazingira Mkoani 

hapo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano 

na Mazingira Mhe. January Makamba ameahidi kujenga 

uwezo kwa watendaji hao kwa kuwapatia mafunzo.

Aidha, Waziri Makamba amesisitiza unaziswaji kwa Kamati 

za Mazingira katika ngazi za vitongoji, vijiji na kata nchi 

nzima na kuahidi kutuma wataalamu kutoa mafunzo kwa 

kamati hizo ili ziweze kujua majumu yao ipasavyo na kusema 

kuwa shughuli za hifadhi za mazingira hazitafanikiwa kama 

Kamati za mazingira hazitatimiza majukumu yake katika 

ngazi hizo.

Waziri Makamba amesema kuwa dunia tunayoishi sasa 

tumeiazima kwa kizazi kinachokuja hivyo hatuna budi 

kuitunza. “Ukiazima kitu kwa mtu yeyote huna budi 

kukitunza na kukulinda ila kukirudisha kwa mwenyewe 

kikiwa katika hali nzuri.” Makamba alibainisha.

Katika wakati mwingine Waziri Makamba ameuagiza 

uongozi wa Mkoa wa Tabora kuteua ama kuajiri Maafisa wa mazingira wa kutosha ili kusimamia kikamilifu uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira, pamoja na kuandaa mpango tekelezi wa mazingira katika ngazi ya Mkoa.

Kuhusu usimamizi wa taka, Waziri Makamba ametoa wito 

kwa uongozi wa Mkoa wa Tabora na Halmashauri zote kuwa 

na takwimu sahihi ya kiwango cha taka kinachozalishwa kwa 

siku ili taka hizo ziweze kutumia katika uzalishaji wa nishati. 

“Naagiza kila Halmashauri kufahamu kiwango cha uzalishaji 

wa taka, hii itasaidia kuja na miradi ya kuzalisha nishati 

mbadala pale fursa zitakapopatikana.” Makamba alisisitiza.

Katika hatua nyingine Waziri Makamba amesisitiza 

matumizi ya nishati mmbada kwa taasisi za Serikalini ili kupunguza kiwango cha ukataji wa miti na matumizi ya mkaa, pia amewataka wadau na wakulima wa tumbaku kubuni namna bora ya kuchoma tumbaku ili iweze kupata soko zaidi duniani. “Sote tunafahamu kuwa miti ni gharama, haiwezekani mkulima kuteketeza kiasi cha miti yenye thamani ya Shilingi laki mbili kuzalisha tumbaku ya elfu themanini, hii haikubaliki ni lazima tubadilishe uchomaji wake”. Waziri Makamba amebainisha.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri 

amemueleza Waziri Makamba jinsi Mkoa wake 

unavyotekeleza kikamilifu kampeni ya upandaji miti kwa 

kuwa na kauli mbiu ya ‘Tabora ya Kijani’ na  amemshukuru 

Waziri Makamba kwa kufanya ziara katika Mkoa wake na 

kuahidi kutekeleza agizo la kuteua maafisa wenye sifa ya 

kuwa wakaguzi wa Mazingira.

Waziri Makamba amehitimisha ziara yake Mkoani Tabora 

kwa kutembelea Bwawa la Igombe na Kazima ili kuona 

utashi na utayari wa wananchi katika kuhifadhi maeneo hayo kabla ya kutangazwa katika gazeti la Serikali kama eneo lindwa. Akiwa Kijijini Igambilo Mheshimiwa Makamba ameahidi kutoa mifuko 100 ya Saruji kuchangia ujenzi wa Zahanati kijijini hapo.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.