Habari za Punde

Arsène Wenger kuelekea Liberia Ijumaa kutunzwa na Rais George Weah

George Weah akiwa pamoja na Arsène Wenger

Rais wa Liberia George Weah anamtunuku kocha wake wa zamani Arsène Wenger, na tuzo la hadhi ya juu zaidi nchini humo.
Rais Weah, mwafrika pekee kuwahi kushinda tuzo la mchezaji bora wa mwaka, alisainiwa Wenger mwaka 1988 wakati akiwa kocha ya klabu ya Monaco.
Wenger, ambaye aliondoka Arsenal kama meneja mwezi Mei baada ya miaka 22 klabuni humo aliwakuza manyota kadhaa kutoka Afrika.
Weah alistaafu kutoka soka mwaka 2003 na kuingia siasa. Alishinda uchaguzi wa mwaka uliopita kwa kura nyingi.
Wenger anaratarajiwa kuwasili mji mkuu wa Liberia Monrovia kupokea tuzo hilo siku ya Ijumaa.
Taarifa hizo zimezua maoni tofauti nchini Liberia huku wengine wakisema kuwa tuzo hiyo hastahili kupewa mtu binafsi kwa kile wamefanya kwa rais.
George Weah, 51, alishinda uchaguzi wa urais mwezi Disemba kwa asilimia 62.
Lakini tuzo hiyo si tuzo kuhusu uhusiano wa Rais na Wenger bali inatambua kile Wengee amechangia kwa michezo barani Afrika na kuwapa waafrika wengi fursa kwa mujibu wa waziri wa habari.
Wenger alikuwa kocha wa wachezaji 16 kutoka Afrika wakiwemo Kolo Toure kutoka Ivory Coast, Mlinzi raia wa Cameroon Lauren, na raia wa Nigeria Nwankwo Kanu
Rais Weah amesema kuwa Wenger "alinitunza kama mtoto wake" wakati alijiunga na Monaco, akisema kuwa "kando na Mungu, anafikiri kuwa bila ya Wenger hakuna vile nigefanikiwa Ulaya".


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.