Habari za Punde

Kutana na mbwa kizingiti mkubwa wa walanguzi wa pembe za ndovu

Asakari wa (KWS) Edwin Koech, akiwa na mbwa Ram wakati wa mafunzo.
Ugunduzi mpya ambao umetajwa kuwa utawapa mbwa uwezo zaidi wa kuwanasa walanguzi utaanza kutumiwa hivi karibuni.
Mfumo huo utawawezesha mbwa kunusa pembe za ndovu na bidhaa zingine haramu za wanyama pori zilizofichwa kwenye kontena kubwa kwa kutumia hewa maalum.
Mfumo huo unafanyiwa majaribio kwenye bandari ya Mombasa, ambayo inatajwa kuwa kubwa zaidi kwa kupitishia pembe za ndovu barani Afrika.

Kulingana na ripoti moja, zaidi ya kilo 18,000 za pembe zilishikwa bandarini humo kati ya mwaka 2009 na 2014.
Kuzalisha kiwango kama hicho, ripoti hiyo inasema kuwa zaidi ya ndovu 2,400 huenda waliuawa na ndicho kiwango tu kilichopatikana.
Mfumo huu utakuwa wenye manufaa makubwa katika kupunguza bidhaa za wanyama pori walio katika hatari ya kuangamia zinazopitia bandarini humo kwenda nchi za ng'ambo.
Uwezo mkubwa wa mbwa wa kunusa unamaanisha kuwa wanaweza kunusa hata kiwango kidogo cha pembe kwenye kontena kubwa ya futi 40.
Magenge ya ulanguzi yanazidi kutumia mbinu ngumu kuficha na kusafirisha bidhaa haramu za wanyama pori.
Ram. mbwa wa kunusa wa shirika la wanyamapori nchini Kenya wakati wa mafunzo mjini Mombasa.
Licha ya kuchukua muda mrefu mfumo huu umefanikisha katika upatikanaji mara 26 ndani ya miezi 6 na kuzipa mamlaka habari muhimu kuhusu mitandao ya wahalifu ambayo hupata mamilioni ya pesa kila mwaka kutokana na biashara haramu.
Mfuko wa wanyama pori duniani WWF unakadiria kuwa ni faru weusi 25,000 waliosalia, na zaid ya 1000 waliuawa na wawindaji haramu nchini Afrika Kusini pekee mwaka huu.
Wakati huo huo makundi wa kulinda wanyama yanakadiria kuwa ndovu 55 wanauawa kila siku kutokana na pembe zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.