Habari za Punde

Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe na Kijitoupele Wakabidhi Magari Matatu kwa Ajili ya Wanafunzi na Shughuli za Kijamii Jimboni.

 
MAGARI matatu yakionekana pichani  yaliyotolewa na Mbunge wa Kijitoupele na Pangawe Shamsi Vuai Nahodha.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘’Mabodi’’ akikata utepe wa kuzinduliwa rasmi kwa magari hayo ambayo ni mabasi mawili ya Wanafunzi wa Majimbo hayo na Canter moja kwa ajili ya shughuli za kijamii.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘’Mabodi’’  akiendesha gari aina ya Canter iliyotolewa na Mbunge huyo.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘’Mabodi’’ akikagua maendeleo ya ujenzi wa Skuli ya msingi ya Kwarara inayojengwa na viongozi wa jimbo hilo.
 MBUNGE wa majimbo ya Kijitoupele na Pangawe, Shamsi Vuai Nahodha akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano ya Maghari hayo.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘’Mabodi’’ akizungumza na wananchi wa majimbo ya Kijitoupele na Pangawe katika hafla ya kuwakabidhi magari matatu ambayo ni mabasi mawili na Canter moja yaliyotolewa na Mbunge wa Majimbo hayo Shamsi Vuai Nahodha.
Na. Is-Haka Omar, Zanzibar.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) 
Zanzibar, Dk.Abdulla Juma Mabodi amewataka Wabunge na 
Wawakilishi nchini kuongeza kasi ya kutatua kero za 
wananchi kwa wakati kama walivyowaahidi katika kampeni 
za uchaguzi mkuu uliopita.
Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kukabidhi magari matatu 
kwa wananchi wa majimbo ya Kijitopele na Pangawe 
ambapoMagari hayo yana thamani ya shilingi milioni 128 
yaliyotolewa na Mbunge wa Majimbo hayo, Shamsi Vuai 
Nahodha.
Akizungumza katika ziara yake ya kutembelea majimbo 
hayo    iliyofanyika katika uwanja wa mpira wa Magirisi 
uliopo Kijitoupele, Dk.Mabodi  alisema huu ndio wakati wa 
viongozi wa majimbo kutekeleza kwa kasi Ilani ya Uchaguzi 
ya mwaka 2015/2020.
Akizungumzia vitendea kazi hivyo ambavyo ni magari 
matatu yakiwemo mabasi ya Wanafunzi mawili na  moja 
ambalo ni Canter kwa ajili ya shughuli za kijamii, aliwambia 
wananchi kuwa wanakiwa kuthamini  juhudi za kiongozi 
huyo aliyetekeleza ahadi yake kwa vitendo.
Dk. Mabodi alieleza kwamba malengo ya Chama Cha 
Mapinduzi ni kuhakikisha wananchi wa mijini na vijijini 
wanaondokana na changamoto mbali mbali za kijamii kabla 
ya uchaguzi mkuu ujao.
Alisema mabasi yaliyotolewa yatawasaidia wanafunzi wote 
wa majimbo hayo bila kujali tofauti za kisiasa.
kiongozi huyo A katika ziara yake ya kutembelea miradi 
mbali mbali ya Chama iliyokutekeleza ahadi walizowaahidi 
wananchi katika kampeni  amesema wananchi wanakiamini 
na kukiunga mkono Chama kutokana na kutatua kwa wakati 
kero zinazowakabili wananchi.
“Miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa 
majimboni na viongozi wa CCM ni kwa ajili ya wananchi 
wote, na tunaomba wananchi muendelee kutuamini na 
hatimaye mwaka 2020 mkichague Chama chetu kiendelee 
kuongoza dola.”, alisema Dk. Mabodi.

Naye Mbunge wa majimbo hayo, Shamsi Vuai Nahodha 
alisema CCM imeendelea kuwa na mvuto kwa jamii 
kutokana na ukweli na dhamira ya dhati ya viongozi wake 
kuwatumikia wananchi kwa vitendo.
Mbunge huyo Naohodha ambaye pia ni Waziri Kiongozi 
Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar alisema kwa 
kushirikiana na viongozi wengine wa majimbo mawili 
anayoyatumikia wamefanikiwa kutatua kero za wananchi 
kwa kiwango kikubwa.
Shamsi alisema na kuongeza kuwa wameimarisha huduma 
muhimu za kijamii zikiwemo upatikanaji wa maji safi na 
salama, ujenzi wa vituo vya Afya pamoja na ujenzi wa shule 
za kisasa za msingi na sekondari.
Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu pia alitembelea ujenzi 
wa Kituo cha Afya katika Jimbo la Kijitoupele ambacho 
kimejengwa kwa ushirikiano wa Mwakilishi wa jimbo hilo, 
Ali Suleiman Ali ‘’Shihata’’  pamoja na Mbunge wa jimbo hilo 
Shamsi Vuai Naohodha  ambacho hadi kukamilika kwake 
kitatumia zaidi ya shilingi milioni 59.
Pia Naibu Katibu Mkuu Dk. Mabodi alitembelea Shule ya 
Sekondari Kwarara na Kituo cha elimu na habari  sambamba 
na kukagua ujenzi wa shule ya msingi ya Kwarara 
itakayotumia shilingi bilioni 1.3 hadi ujenzi wake kukamilika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.