Habari za Punde

Mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora Kati ya Mafunzo na Opec Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Mafunzo Imeshinda Bao 3-1.

Mshambuliaji wa Timu ya Opec kutoka Pemba Khamis Sadik akiruka kihuzi cha beki wa Timu ya Mafunzo Abdulmalik Adam akiwa chini, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Mafunzo imeshinda mchezo huo kwa bao 3-1.

Katika mchezo huo uliofanyika katika wa Amaan Zanzibar hatua za mzunguko wa pili uliozikutanisha timu hizo katika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Mafunzo imeandika bao lake la kwanza kupitia katika dakika ya kwanza ya mchezo huo kupitia mshambuliaji wake Said Mussa. Timu ya Opec imeweza kusawazisha bao lake katika kipindi cha kwanza katika dakika ya 23 kupitia mshambuliaji wake Daudi Yussuf.

Dakika mbili baada ya Opec kusawazisha waliweza kujisahau na katika dakika ya 26 ya mchezo huo kipindi cha kwanza mshambuliaji wa Timu ya Mafunzo Amour Abdallah, akaipatia timu yake bao la pili, hadi mapumziko timu hizo zimetoka uwanja Tmu ya mafunzo ikiongoza kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili ca ha mchezo huo kilikuwa na mashambuliza katika lango la Timu ya Mafunzo lakini juhudi hizo hazijazaa matunda na katika dakika ya 81 ya mchezo huo kipindi cha pili mshambuliaji wa Mafunzo Ali Othman ameiandikia timu yake bao la tatu na la mwisho katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.