Habari za Punde

Sherehe za Siku ya Kizimkazi Day Mgeni Rais Mhe. Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Awataka Wananchi wa Kizimkazi Kuuenzi Utamaduni Wao.

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mzee wa Kamati ya Siku ya Kizimkazi Dar na kushoto Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hassan Khatib Hassan wakielekea katika viwanja vya Tamasha la Siku ya Kizimkazi Day baada ya kupata vyakula vya Asili ya Kusini Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa bendera na mmoja wa Vijana walioshiriki Matembezi kuadhimisha Siku ya Kizimkazi Day, wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya Kizimkazi Mkunguzi Mkoa wa Kusini Unguja Wilaya ya Kusini.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hassan Khatib Hassan akizungumza na kutowa mnaelezo ya Sherehe hizo za kila mwaka za Siku ya Kizimkazi Day, zilizofanyika katika viwanja vya mkunguni Kizimkazi Wilaya ya Kusini Unguja.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hassan Khatib Hassan akimkabidhi Nembo ya Siku ya Kizimkazi Day Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman. Nembo hiyo itatumika kwa machapicho ya matangazo mbalimbali na fulana kwa ajili ya kuitangaza Kizimkazi Day kwa wageni na Wananchi wa Tanzania. 
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhia machapisho ya Fulana zenye nembo ya Siku hya Kizimkazi Day wakati wa hafla ya sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya Mkunguni Kizimkazi Wilaya ya Kusini Unguja.
Waziri wa Michezo Vijana Sanaa na Utamaduni Mhe. Balozi Ali Karume akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Kijiji cha Kizimkazi wakati wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Kizimkazi Day zilizofanyika katika viwanja vya mkunguzi Kizimkazi Wilaya ya Kusini Unguja
Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman akizungumza wakati wa hafla hiyo kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzungumza na wananchi wa Kizimkazi Wilaya ya Kusini Unguja. 
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Kizimkazi wakati wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Kizimkazi Day zilizofanyika katika Kijiji cha Mkunguni Wilaya ya Kusini Unguja Mkoa wa Kusini, na kusisitiza ushirikiana na kudumisha ushirikiano wa Wananchi wa Vijiji hivyo vitatu katika kudumisha utamaduni wao. 
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisisitiza jambo wakati akiwahutubia Wananchi wa Kizimkazi Wilaya ya Kusini Unguja wakati wa sherehe za Siku ya Kizimkazi Day zilizoadhimishwa kwa michezo mbalimbali ya ufutaji kamba michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete na resi za ngalawa.
Wananchi wa Kijiji cha Kizimkazi wakivuatilia hafla ya sherehe za kuadhimisha Siku ya Kizimkazi Day katika viwanja vya Mkunguzi Kizimkazi Wilaya ya Kusini Unguja.

Wananchi wa Kijiji cha Kizimkazi wakivuatilia hafla ya sherehe za kuadhimisha Siku ya Kizimkazi Day katika viwanja vya Mkunguzi Kizimkazi Wilaya ya Kusini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.