Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akikagua maeneo ya
Kisiwa cha Magafu, takribani mwendo wa dakika thelathini kutoka mwalo wa Nyamirembe.
Waziri Makamba aheahidi kutuma wataalamu ili kujiridhisha zaidi kabla ya
kutanga katika gazeti la Serikali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na wakazi
wa kijiji cha Nyamirembe juu ya utayari wao wa kuhifadhi mazingira ya Kisiwa
hicho ili kuwa miongoni mwa maeneo yanayopendekezwa kulindwa kwa mujibu wa
Sheria ya Mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwasilkiliza wakazi
wa kijiji cha Nyamirembe juu ya utayari wao wa kuhifadhi mazingira ya Kisiwa
hicho ili kuwa miongoni mwa maeneo yanayopendekezwa kulindwa kwa mujibu wa
Sheria ya Mazingira.
Na.Lulu Mussa.
Siku ya Sita ya ziara ya
Waziri Makamba imemfikisha Mkoani Geita, Wilayani Chato katika Kijiji cha
Nyamirembe ambapo pamoja na mambo mengine Mhe. Makamba ametembelea Kisiwa cha
Magafu na kuahidi kutuma timu ya wataalamu kwa ajili ya kufanya tathmini ya namna
ya kulinda kisiwa hicho kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, ikiwa
ni eneo tengefu kwa mazalia ya samaki.
Akiongea na Uongozi wa
Mkoa wa Geita Waziri Makamba amesema kuwa jitihada za Serikali ni pamoja na
kuhakikisha ulinzi madhubuti kwa kisiwa hicho ili kiwe kielelezo cha
mandhari
tulivu kwa mazalia ya samaki na bioanuai.
Waziri Makamba amesema
kuwa hakuna sekta yoyote muhimu kwa uchumi wa nchi isiyohitaji Hifadhi ya Mazingira hivyo Sheria ya Mazingira kifungu namba 51 inatoa mamlaka na nafasi
ya kulinda maeneo nyeti na kuainisha kuwa kuna dhana potofu kuwa uhifadhi wa mazingira ni kinyume na maendeleo.
Dhana ya uhifadhi
inaendana na utashi, uwezo, utayari na ushirikishwaji wa wananchi wenyewe.
“Tunapoongelea uhifadhi tunaamanisha, kuweka utaratibu wa kutumia maeneo
yaliyopendekezwa kuhifadhiwa kwa taratibu zitakazopendekezwa, mfano kama
tunahifadhi kisiwa, tutaweka utaratibu maalumu wa uvuaji wa samaki katika eneo
hilo” Makamba alisisitiza.
Pamoja na mambo mengine
Waziri Makamba amesema Ofisi yake iko tayari kuteua wakaguzi wa mazingira kadri iwezekanavyo na kutoa mafunzo kwao pindi majina yatakapowasilishwa kwake na
Sekretarieti ya Mkoa.
Awali Mkuu wa Mkoa wa
Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi
amesema kuwa Mkoa wake kwa asilimi 35 umezungukwa na madini na kupelekea
uharibifu wa Mazingira kutokana na shughuli za uchimbaji hata hivyo Ofisi yake
imekuwa ikifanya ukaguzi wa mara kwa mara katika shughuli za uchenjuaji kwa
kuhakikisha usalama wa afya za watu na mazingira.
Akielezea jitihada za Mkoa
wake katika suala la kuhifadhi mazingira Mhandisi Gabriel amesema wamekuwa na mwendelezo wa kampeni ya upandaji miti kwa kila Halmashauri zote na kutunza
miti ya asili, ikiwa ni pamoja kuondoa wavamizi haramu katika misitu,
operesheni ambayo ni endelevu. “Huwezi kutenganisha mazingira na uhai wa watu”
Mhandisi Gabriel alisisitiza.
Waziri Makamba yuko katika
ziara ya kikazi katika Mikoa tisa (8) nchini yenye lengo la kukagua, kutathmini
na kuzungumza na viongozi kuhusu maeneo yanayopendekezwa
kuhifadhiwa kwa mujibu
wa Sheria ya Mazingira kifungu namba 51.
No comments:
Post a Comment