Habari za Punde

Ziara ya Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Khalid Kutembelea Miradi ya Uchimbaji wa Mitaro ya Maji Machafu Maeneo ya Unguja.Inayojengwa na Kampuni Kutoka China ya CRJE.

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Mohammed Salum akipata maelezo ya michoro ya Ujenzi wa Jaa katika Kijiji cha Kibele wakati wa ziara yake kutembelea Miradi ya ZUSP Zanzibar.
Pia ametembelea eneo linalotarajiwa kujengwa Jaa jipya na la kisasakatika eneo la Kibele Nje Kidogo ya Mji wa Unguja Wilaya ya Kati. Mkoa wa Kusini Unguja.Miradi hiyo inasimamiwa na Mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP) akiwa katika eneo linalotaka kujengwa jaa la kisasa kupitia Mradi huo.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Mohammed Salum akipata maelezo ya Michero ya Mradi wa Ujenzi wa Jaa la Kisasa katika eneo la Kibele Unguja wakati wa ziara yake kutembelea Miradi ya ZUSP Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Mohammed Salum akipata maelezo ya ramani ya Mtaro wa Maeneo ya Mpendae unaounganishwa na Mtaro wa Jangombe na Magomeni kupitishia maji hayo. 

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Mohammed Salum akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara yake katika Miradi ya ZUSP inayosimamia Ujenzi wa Mitaro ya Maji katika maeneo ya Chumbuni, Mpendae, Jangombe na Magomeni Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.