Habari za Punde

Mbunge wa Viti Maalum Kupitia UVCCM Kisiwani Pemba Mhe. Munira Mustafa Afanya Ziara Kutembelea Matawi ya Vijana wa UVCCM Micheweni Pemba.

Mbunge wa Viti Maalum Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mhe. Munira Mustafa Khatib, akizungumza na Viongozi wa Jumuiya ya Vijana wa CCM, Wilaya ya Micheweni -Pemba, wakati wa ziara yake ya kuhamasisha Vijana katika Matawi ya Jumuiya hiyo Kisiwani Pemba.
Mwenyejiti wa UVCCM, Mkoa wa Kaskazini Pemba , Yahya Khamis Ali,akifunguwa mkutano wa Jumuiya hiyo ulioitishwa na Mbunge wa viti maalumu UVCCM Taifa.
Wajumbe wa UVCCM , Wilaya ya Micheweni Pemba,wakiwa katika mkutano wa Pamoja baina yao na Mbunge wa viti maalumu Vijana , Munira Mustafa Khatib, huko katika Wilaya ya Micheweni.

Mjumbe wa UVCCM Wilaya ya Micheweni Hamad Sule Hamad, akichangia jambo katika mkutano wa Mbunge wa Viti maalumu UVCCM Pemba, Munira Mustafa Khatib katika kuangalia utendaji wa jumuiya hiyo Kisiwani Pemba.
Picha na Habiba Zarali - Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.