Habari za Punde

Mabingwa wa Tanzania Simba Sports Club Yalazimishwa Sare na Timu ya Ndanda FC Mchezo wa Ligi ya Tanzania Bara

Mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Ndanda dhidi ya mabingwa watetezi Simba umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

Hii ni mara ya kwanza kwa klabu ya Ndanda kupata pointi moja dhidi ya Simba kwani tangu ipande daraja misimu minne iliyopita haikuwa imewahi kushinda wala kupata sare dhidi ya Simba.

Licha ya kumiliki mpira kwa muda mwingi washambuliaji wa Simba John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi hawakufanikiwa kuipenya ngome ya Ndanda iliyotumia wachezaji wote 10 katika kujilinda.

Matokeo ya michezo yote iliyopigwa leo;

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.