Habari za Punde

MAMBO MATANO YA KUZINGATIA UNAPONUNUA NGUO ZA MTOTO MCHANGA

Na Jumia Tanzania.
Kama una mtoto mchanga au unatarajia, hususani ikiwa ni kwa mara ya kwanza,
lazima utakuwa unakumbana na changamoto ya kujua ni nguo za aina gani zitakazomfaa.
Wazazi wengi huwa wanasisimka na ujio mpya wa mtoto wao hivyo kupelekea kununua
chochote kila watakachokiona kinawavutia mbele ya macho yao.
Hata hivyo, Jumia ingepependa kukushauri wewe kama mzazi wa mtoto, ndugu au jamaa
ambaye una mpango wa kununua nguo kuwa makini na kuzingatia kununua zile ambazo
zitamtosha mtoto na kujisikia raha mustarehe.

Yakupasa kutokununua vitu ambavyo hautakuja kuvitumia au havitomfaa mtoto au nguo
ambazo utakuwa umepoteza pesa zako bure. Miongoni mwa mambo unayopaswa
kuyazingatia pindi unaponunua nguo za watoto wachanga ni pamoja na ulaini wake,
umadhubuti, na usalama. Katika hatua hii suala la kuzingatia mavazi yanayotengenezwa
na wabunifu mbalimbali usilipe uzito mkubwa.    

Sio kila mtu anao uzoefu wa kununua nguo za watoto hususani watoto wachanga.
Ulikuwa unajiuliza ni mambo gani ya kuzingatia pindi unapokwenda dukani? Yafuatayo
ni masuala ya msingi kuyafahamu na kuzingatia:

Sio lazima ununue nguo za wabunifu. Hakuna asiyevutiwa na nguo za wabunifu wa
mavazi kutokana na ubora wake pamoja na mitindo tofauti. Jambo la msingi ambalo unatakiwa
kulifahamu ni kwamba watoto wachanga hutumia muda mwingi kulala na hukua
kwa haraka. Kwa hiyo, itakuwa ni kupoteza pesa kuwekeza katika kununua nguo nyingi
ambazo mtoto wako hatozivaa. Ni vema kusubiria angalau mtoto akue kidogo ndipo
ununue hizo nguo kwani atakuwa na muda wa kuzivaa kwa muda mrefu.      
Zingatia kununua nguo zitakazomfanya astarehe. Kama mtu mwingine yeyote, mtoto
mchanga pia hupenda kuwa katika mazingira anayojisikia vizuri muda wote. Hivyo basi
unavyofikiria kumnunulia nguo zingatia zile zitakazomfanya ajisikie vizuri muda wote.
Hii itampelekea kulala vizuri bila ya usumbufu hata na wazazi au walezi nao pia watapata
muda wa kupumzika.

Watoto wachanga hutumia muda mwingi kulala. Watoto wachanga hutumia mpaka
masaa 18 kulala kwa siku! Hii ina maana kwamba katika manunuzi yako ya nguo hakikisha
kwamba unanunua zile ambazo zitamfanya ajisikie vizuri pindi alalapo.   
Utapokea zawadi nyingi za nguo. Sehemu tofauti duniani kuna kawaida ya kumfanyia
sherehe mama mjamzito kipindi anapokaribia kujifungua. Kutokana na maendeleo kwenye
sekta ya huduma ya afya kwa sasa, wazazi wengi hujua jinsia ya mtoto au watoto
atakaojifungua. Sherehe hizi huambatana na zawadi nyingi zikiwemo nguo pamoja na vitu
mbalimbali kwa ajili ya mtoto atakayezaliwa. Hivyo basi, unashauriwa kabla ya kununua
nguo za watoto ni vema ukasubiria matukio kama haya kupita ili usije kununua vitu ambavyo
unaweza kuzawadiwa.   
Zingatia saizi ya nguo za mtoto. Kama umeshawahi kusikia kuwa watoto wachanga
wanakua kwa haraka amini ni kweli! Si jambo la kushangaza mtoto mchanga utakayemuona
siku anazaliwa utashangaa kumkuta amebadilika mno baada ya mwezi mmoja tu. Kwa hiyo,
unapofanya manunuzi ya nguo lazima uzingatie suala la ukuaji wa haraka wa
mtoto la sivyo utajikuta unanunua nguo ambazo baada ya muda fulani hazimtoshi.
Wazazi wanashauriwa kununua nguo ambazo ni mara mbili ya saizi ya sasa ya mtoto.
Na unashauriwa kufanya hivyo angalau mpaka mtoto afikie umri wa miaka miwili na
kuendelea ndipo ununue nguo za saizi yake halisi.
Katika kurahisisha manunuzi ya nguo na vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto, Jumia inayo
mahitaji yote kwa ajili yakoi. Kutokana na kutingwa na majukumu mengi muda wa kwenda
madukani na kuchagua nguo zitakazo mfaa mtoto huwa ni mdogo. Lakini kupitia
Jumia unaweza kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao mahali na muda wowote ulipo
kisha ukaletewa bidhaa zako mpako ulipo. Bidhaa ni nyingi na zinapatikana kwa bei nafuu,
unaweza kutembelea sasa tovuti yao.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.