Na.Raya
Hamad OR KSUUUB
Waziri nchi
Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Haroun Ali
Suleiman amesema kuwa demokrasia na Utawala bora ni nyenzo muhimu katika ujenzi
wa jamii yenye umoja mashirikiano
uwadilifu na uwajibikaji ambao hujenga heshima na nidhamu katika utekelezaji wamajukumu
ya kazi
Waziri Haroun
ameyasema hayo alipokutana na watendaji wakuu na wafanyakazi wa Ofisi ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika
muendelezo wa ziara za kutembelea
taasisi zilizomo ndani ya Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na
Utawala Bora
Utekelezaji wa kazi za majukumu ya Serikali unazingatia misingi ya utawala bora kama
ilivyoainishwa katika Katiba za nchi na kuimarisha uwazi na uwajibikaji kwa wananchi hivyo amewahimiza watendaji hao kutokubali
kutumiwa vibaya au kurubuniwa kwa njia yoyote
katika kutekeleza wajibu wao
“Ofisi ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali ni taasisi ambayo imepewa
dhamana maalum na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hivyo suala la kujituma
na kufuata maadili ya kazi ni lazima
msije mkababashwa fanyeni kazi wala hakuna kupotea kwa fedha ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar fuateni
taratibu zote za ukaguzi kwa mujibu wa sheria na Katiba ya nchi kama
inavyoelekeza ”
Aidha Waziri
Haroun amewaasa vijana waliopata ajira hivi karibuni kutojiingiza katika
masuala ya Siasa katika utendaji wao wa kazi na kusoma vizuri sheria ya
utumishi ili kuelewa kanuni na taratibu
za utumishi pamoja na kufuata muongozo
na majukumu yao kazi
wanazopangiwa jambo ambalo litaleta
ufanisi wa Ofisi hio
Nae Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Bi Fatma
Mohammed Said amesema kuwa Ofisi
hio inatekeleza majukumu yake Kikatiba na kwa kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya
CCM 2015 -2020 na kusisitiza kuwa Katiba
ya Zanzibar 1984 kifungu 112 (3) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
hesabu za Serikali anawajibika
“kuhakikisha kwamba fedha zote zinazokusudiwa
kutolewa kutoka Mfuko wa Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
matumizi yake yameidhinishwa kisheria na iwapo atatosheka kwamba masharti hayo
yatatekelezwa ipasavyo basi ataidhinisha fedha hizo zitolewe ”
Aidha
kifungu B kinazungumza kuwa kuhakikisha
kwamba fedha zote amabazo matumizi yake yameidhinishwa yanatokana na fedha
zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au fedha
ambazo matumizi yake yameidhinishwa na sheria iliyotungwa na Baraza la
Wawakilishi na ambazo zimetumika katika
shughuli iliyokusudiwa na matumizi ya fedha hizo yamefanywa kwa kufuata idhini
iliyotolewa kuhusu matumizi hayo
Angalau mara
moja kwa mwaka kufanya ukaguzi na kutoa taarifa
juu ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hesabu zinazosimamiwa na watumishi wote wa
Serikali ya Mapinduzi ya Mapinduzi ya Zanzibar , Hesabu za Mahakama zote za Zanzibar, Hesabu za Tume
au vyombo vyengine vilivyoidhinishwa na Katiba hii na hesabu zinazohusika na Baraza la Wawakilishi
Bi
Fatma amesema Ofisi inaendelea kufanya
kazi za ukaguzi wa hesabu katika Wizara zote za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
Maidara , Taasisi, Mamlaka , Mashirika na miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na
washirika wa maendeleo na kutoa ripoti za Ukaguzi wa hesabu hizo na kuwasilishwa kwa mujibu wa Katiba .
“Ripoti hizo
zimekuwa zikifanyiwa kazi na Serikali
ikiwemo Kamati ya Kudhibiti na Kuchunguza Hesabu za Serikali (PAC)”alisisitiza
Ofisi ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali pia
inaendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa mujibu wa Ibara ya
143(a)Ofisi ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali
inashirikiana na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania katika kufanya ukaguzi wa pamoja katika miradi mbalimbali ya maendeleo
ikiwemo Miradi ya Umoja wa Mataifa , Benki ya Dunia , Benki ya Maendeleo ya
Afrika nk
Kupitia
mashirikiano yaliyopo ya taasisi hizo Ofisi imefanikiwa kuimarisha mashirikiano
na wadau mbali mbali wa ndani na nje kupitia mafunzo , mikutano semina , makongamano na warsha mbali mbali
kitaifa na kimataifa
Akielezea
baadhi malengo iloyojipangia Ofisi hio
Bi Fatma amesema ni pamoja na kuendelea
kutekeleza majukumu Kikatiba ya Ukaguzi wa Hesabu , kuendelea kuimarisha uwezo
wa wafanyakazi kitaaluma katika fani
mbali mbali za Ukaguzi kama vile ukaguzi wa matokeo ya utekelezaji wa
program(PBB AUDIT) ukaguzi wa mazingira , ukaguzi wa komputa , ukaguzi yakinifu
na ukaguzi wa aina nyenginezo
Kutoa
mafunzo ya ukaguzi wa hesabu unaozingatia viwango vilivyowekwa kitaifa na
kimataifa , kutoa mafunzo ya mabadiliko ya teknologia katika mifumo ya uhasibu
na ukaguzi na mafunzo ya mabadiliko ya Bajeti kwa wakaguzi kutoka katika mfumo
wa vifungu (line iterm) kwenda mfumo
unaozingatia matokeo (PBB)
Katika
kutekeleza majukumu na kuimarisha
Ofisi inatumia vifaa vya kisasa pamoja
na kuongezeka kwa wafanyakazi wenye taaluma ambapo wafanyakazi wapya 87
wameajiriwa na kupatiwa mafunzo ya awali yakiwemo mafunzo ya sheria na kanuni
za utumishi wa Umma ,usalama wa Afya, kazini , maadili ya Utumishi wa Umma
pamoja na sheria za kutunza siri ili
kuongeza ufanizi na kuifanya Ofisi hio kuwa na jumla ya wafanyakazi 215
Hata hivyo
Bi Fatma amesema zipo baadhi ya changamoto ambazo zinaendelea kupatiwa ufumbuzi
mara tu zinapojitokeza lakini baadhi zinahitaji rasilimali kubwa ili ziweze
kutatuliwa ikiwemo mabadiliko ya Teknolojia na mifumo ya fedha, uhasibu na
ukaguzi
“kwa kuwa
utekelezaji wa kazi za ukaguzi unakabiliwa na mabadiliko ya mara kwa mara Ofisi
inaendelea na uratibu wa kuwajengea uwezo wafanyakazi wake kwa kuwapatia
mafunzo ya muda mfupi na mrefu il kuendana na teknologia habari na mawasiliano
kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kazi za ukaguzi ” alisema
Ofisi ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali ni Taasisi ya Katiba
inayojitegemea ambapo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali ndio
kiongozi mkuu wa Ofisi anaesimamia shughuli za uongozi na uendeshaji
No comments:
Post a Comment