Habari za Punde

Michuano ya Kombe la Bonaza la Timu ya Ujamaa Sports Club Timu ya Taifa ya Jangombe Yaingia Nusu Fainali Baada ya Kuifunga Timu ya Raskazone. Kwa Mikwaju ya Penenti 4 -3.Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe kushoto Feysal Hilal akimpita beki wa Timu ya Raskazone Bakari Amani wakati wa mchezo wao wa Robo Fainali ya Michuano ya Bonaza la Timu ya Ujamaa mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Taifa ya Jangombe imeshinda mchezo huo kwa penenti 4-3.

Timu ya Taifa ya Jangombe imefanikiwa kusonga mbele baada ya kuifnga Timu machachari ya Raskazone ilioko Daraja la Pili Taifa kwa mikwaju ya penenti, mchezo huo uliokuwa na ufundi wa kila timu ikionesha jinsi inavyoweza kusakata soka.
Timu ya Raskazone imeandika bao lake la kwanza katika dakika ya saba ya mchezo huo kipindi cha kwanza baada ya mshambuliaji wake kufanyiwa fauli na mlinda mlango wa Timu ya Taifa ya Jangombe na muamuzi wa mchezo huo kuamuru adhabu ya penenti iliopigwa na Abdallah Yahya na kuiandikia timu yake bao la kuongoza.
Nao Vijana wa Wakombozi wa Ngwambu waliweza kuonesha ubabe wao kwa Timu hiyo na katika dakika ya 38 ya mchezo huo kipindi cha kwanza waliweza kusawazisha bao hilo kipitia mshambuliaji wake Said Ali. hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Timu hizo zikiwa sare ya bao 1-1.
Hadi kipindi cha pili cha mchezo huo kinamalizika timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1, na kuamuliwa kupigwa penenti, nayo Timu ya Taifa ya Jangombe ikaibuka mshindi wa mchezo huo. 
Kwa sasa Timu ya Taifa ya Jangombe inasubiri mchezo katri ya Malindi na Mlandege ili kucheza mchezo wa Nusu Fainali ya Michuano hiyo ya Bonaza la Timu ya Ujamaa Sports Club kutimiza miaka 61 tangu kuazishwa kwake mwaka 1957 Zanzibar.    























No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.