Habari za Punde

RC Shigella Awaonya Wananchi wa Kipumbwi Kuhusu Uingizaji wa Dawa za Kulevya na Biashara za Magendo.

 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwakibuyu Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani wakati wa ziara yake ambapo aliwataka kuacha kushiriki kwenye vitendo vya biashara haramu za magendo na uingizaji wa dawa za kulevya
 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso akizungumza katika ziara hiyo ya mkuu wa mkoa
 MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah  Issa akizungumza katika ziara hiyo
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis Mnegero akizungumza katika ziara hiyo
 Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwl Hassani Nyange akizungumza katika ziara hiyo
 Mwenyekiti wa Halmashuri ya wilaya ya Pangani  akizungumza katika ziara hiyo
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katika akiteta jambo na Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gipson kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa wakati wa ziara yake wilayani humo kushoto ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mbunge wa Jimbo la Pangani  (CCM) Jumaa Aweso
 AFISA Tawala wa wilaya ya Pangani Gipson kulia akiwa na wananchi wa Kijiji
cha Kwakibuyu kata ya Kipumbwi wakimsikiliza kwa umakini mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakati wa ziara yake
 Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikilizaa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Kwkibuyu wilayani Pangani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) ambao hawapo pichani wakati wa ziara ya Mkuu wa mkoa huyo


Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amewaonya wananchi wa Kijiji cha Kwakibuyu kata ya Kipumbwi wilayani Pangani wanaojishughulisha na uingizwaji wa dawa za kulevya ,wahamiaji haramu na biashara za magendokuacha mara moja vitendo hivyo kabla hawajakumbana na mkono wa sheria huku akiwataka wananchi kuwafichua watu hao.



Eneo la Kipumbwi limekuwa likitajwa kuwa ni miongoni mwa maeneo ambayo kumekuwa bandari bubu ambayo imekuwa ikitumika kwenye matumizi mbalimbali ikiwemo kuingiza bidhaa za magendo, wahamiaji haramu jambo
ambalo alisema linapaswa kukomeshwa.

Shigella aliyasema hayo jana wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo kuzungumza na wananchi kwenye mikutano ya hadhara wilayani Pangani ambapo alisema Bandari hiyo bubu zimekuwa tatizo
kwenye kutumika kwenye matumizi ambayo yasiyokuwa salama.

“Hapa Kipumbwi mmekuwa na tatizo kubwa la bandari bubu ambayo imekuwa kutumika kwenye matumizi yasiyosalama biashara haramu ya kupitisha wahamiaji, dawa za kulevya ama kusafirisha wahamiaji haramu lakini wapo  baadhi yenu wanadhamira njema ya kuleta bidhaa kutoka maeneo mengine  ikiwemo mkoani Tanga wakati mwengine kivuko kikiwa kimefungwa kinawaongeze gharama watumiaji wa mwisho”

Mkuu huyo wa mkoa wa Tanga alisema pia yapo baadhi ya maombi ya muda mrefu ambayo viongozi wa wilaya hiyo walikwisha kuwasilisha akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo Jumaa Aweso ambaye ni Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji na Mkuu wao wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa.

“Hivyo wataona uwezekano wa kuanzishwa mchakao wa eneo hilo kuwa bandari ndogo na sasa wameanza mchakato kuifanya Kipumbwi iwe bandari ndogo na Meneja wa Bandari ya Tanga alifika kufanya mkutano na DC kuanza mchakato wa kuirasimisha”Alisema

Alisema baada ya kumalizika mchakao wa kuanzishwa bandari ndogo eneo hilo wananchi wapaswa kuhakikisha wanawafichua wale wanaopitisha bidhaa haramu za magendo na kuichafua sura ya kipumbwi kwa kupitisha
dawa za kulevya.

“Kwani tukifanya hivyo tutakuwa tumepiga hatua na dhamira ya kuanzishwa bandari hiyo itakuwa imekamilika lakini ikibainika eneo hilo bado wanapitisha wahamiaji haramu, bidhaa za magendo na dawa za
kulevya hawatasita kuifunga”Alisema RC Shigella.

Naye kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso alisema katika kipindi chake cha miaka miwili amesaidia Jimbo hilo ambalo lina kata 14 kupata umeme wa uhakika ambao ndio wilaya ya kwanza Tanzania ambayo kuna umeme kwenye karibia ya maeneo yote isipokuwa machache tu.

Alisema pia Jimbo hilo miaka ya nyumba lilikuwa likipokea bajeti ya maji milioni 500 mwaka mzima lakini hivi sasa imepanda na kufiikia Bilioni 2 hali ambayo ni jambo jema kwao kwa ustawi wa sekta hiyo muhimu.

“Pamoja na mambo hayo waswahili wanasema lakini niwaambie mpango tulionao kukabiliana na changamoto ya maji tutachimba visima virefu zaidi ya kiwanja cha mpira Kipumbwi na Sakura kuhakikisha wananchi
wanaondokana na tatizo la maji”Alisema.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.