Habari za Punde

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid Akabidhi Mashine ya Kukatia Karatasi na Kuchonga.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid kushoto akimkabidhi mashine ya kukatia karatasi na kuzichonga (Paper Polar 66) Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.  
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiwa ameishika mashine ya kukatia karatasi na kuzichonga (Paper Polar 66) baada ya kukabidhiwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar, wakishuhudia Viongozi wa Wizara na wa Kiwanda cha Uchapaji Zanzibar.

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya kale Mahmoud Thabit Kombo akizungumza baada ya kukabidhiwa Mashine ya Kukatia Karatasi na kuzichonga(PAPER POLAR 66)Katika hafla iliofanyika Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.kulia yake ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Upigaji Chapa (ZAGPA)Mwengine ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Khadija Bakari Juma na wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Upigaji Chapa(ZAGPA)Zanzibar.

Picha na Yussuf Simai -Maelezo Zanzibar)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.