Habari za Punde

Bingwa wa Michuano ya Mimi na Wewe Ndondo Cup 2018 Timu ya Juve.

Mgeni Rasmin Michuano ya Mimi na Wewe Ndondo Cup Mhe. Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akimkabidhi Ngao ya Ushindi wa Kwanza Bingwa wa Michuano hiyo Nahodha wa Timu ya Juventus kutoka Meli Nne Mwanakwerekwe Hassan Madarasi, baada ya kuibukwa Mabingwa wa Michuano hiyo kwa kuifunga Timu ya Six Centers ya Mwera Unguja, mchezio huo uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar..
Na kuhudhuriwa na Wananchi wengi wapenda soka Zanzibar na kufurika uwanja huo.Mgeni Rasmin wa Fainali ya Michuano ya Mimi na Wewe Ndondo Cup Mhe Zuberi Ali Maulid akimkabidhi zawadi ya Ushindi wa Pili wa Michuano hiyo Nahodha wa Timu ya Six Center Haji Idrissa.kulia Mlezi wa Timu hiyo Mwakilishi wa Jimbo la Mwera Mhe. Mihayo Juma Nhunga.


Mgeni rasmin wa Fainali ya Michuano ya Mimi na Wewe Ndondo Cup Mhe. Zuberi Ali Maulid akimkabidhi zawadi yake Kipa Bora kutoka Timu ya Juventar. 
Mgeni Rasmin wa Fainali ya Michuano Mimi na Wewe Ndondo Cup Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akimkabidhi zawadi yake Mshangiliaji Bora wa Michuano hiyo.
 Kipa Bora wa Michuano ya Mimi na Wewe Ndondo Cup akikabidhiwa zawadi yake na Mgeni Rasmin Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Mhe. Zuberi Ali Maulid. 
 Muandishi Bora wa Michuano ya Kombe la Mimi na Wewe Ndondo Cup kutoka Kituo cha Redio cha ZBC Ndg. Abubakari Kisandu.akikabidhiwa zawadi yake na Mgeni Rasmin Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid. Kiongozi wa Timu ya Mwera akikabidhiwa Seti ya Jezi kutokana na mchango wao wakati wa michuano hiyo kutowa Uwanja wao kufanikisha Michuano hiyo tangu kuaza na kufikia tamati katika Uwanja wa Amaan kumalizia mchezo wa Fainali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.