Habari za Punde

Hafla ya Utiaji wa Saini ya Mkataba wa Makubaliano Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asili Zanzibar na Kampuni ya RAKGAS ya Ras Al Khaimah.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mtawala wa Ras Al Khaimah Sheikh. Saud Bin Saqr Al Qasim, wakishuhudia hafla ya utiliaji wa Saini Mkataba wa Mgawanyo wa Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia (PSA) Wakitia saini Waziri wa Ardhi Maji Mazingira na Maakazi Zanzibar Mhe. Salama Aboud Talib katikati na kulia Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta Zanzibar,Bi. Mwanamkaa Abdulrahman Mohammed,Mkurugenzi Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa RakGas Mr.Kamal Mohammed Ataya, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar. 
Wawakilishi wa Serikali ya Mtawala wa Ras Al Khaimah wakifuatilia hafla hiyo ya Utiaji wa Saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asili Zanzibar , iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na mgeni wake Mtawala wa Ras Al Khaimah Sheikh Saud Bin Saqr Bin Qasim, wakifuatilia hafla hiyo ya Utiaji wa Saini katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, wakipongezana na Mtawala wa Ras Al Khaimah Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasim, baada ya utiaji wa sainui hiyo baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Kampuni ya Uchimbaji ya Mafuta ya Rakgas ya Ras Al Khaimah, katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia hafla hiyo ya utiaji wa Saini katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.23/10/2018.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.