Habari za Punde

Mtawala wa Ras Al Khaiman Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasim, Awasili Zanzibar leo Kuhudhuria Hafla ya Utiaji wa Saini Ikulu Zanzibar.

Ndege iliomchukua Mtawala  wa  Ras Al Khaiman Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasim ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kuhudhuria hafla ya Utiaji wa Saini ya Mkataba wa Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia (PSA) 
Mtawala Ras Al Khaiman Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasim akishuka katika Ndege iliomleta kuhudhuria hafla ya Utiaji wa Saini ya Mkataba wa Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia (PSA) akiwa na Balozi wa UAE Nchini Tanzania Balozi Mohammed Al Hammad.baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo jioni kuhudhuria hafla hiyo inayofanyika Ikulu usiku huu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu akisalimiana na Mtawala wa Ras Al Khaiman Sheikh Saud Bin Saqr Al Saqim alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kuhudhuria hafla ya utiaji wa Saini ya Mkataba wa Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia (PSA) inayofanyika katika viwanja vya Ikulu usiku huu.
Mtawala wa Ras Al Khaiman Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasim akipokea heshima ya mapokezi ilioandaliwa na Bwaride rasmin la mapokezi la Jeshi la Wananchi wa Tanzania, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.kuhudhuria hafla ya Utiaji wa Saini ya Mkataba wa Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia (PSA)
Mtawala wa Ras Al Khaiman Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasim akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu wakipita mbele ya gwaride rasmin lililoandaliwa kwa ajili ya mapokezi yake alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Mtawala wa Ras Al Khaiman Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasim akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.