Habari za Punde

Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani Yanayofanyika Kisiwani Pemba.Katika Viwanja Vya Chanamangwe Wilaya ya Wete.

Matikiti ambayo yanalimwa na Jeshi la kujenga Uchumi (JKU) Pemba, ambayo yako katika mabanda ya maonesho ya siku ya Chakula Duniani huko Chanamangwe Wilaya ya Wete Pemba.
Bidhaa  zilizomo katika moja ya mabanda ya JKU yalioko kwenye maonesho ya siku ya Chakula Duniani huko Chamanangwe Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,Mhe.Omar Khamis Othman,akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya Viongozi wa waliogatuliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Idara maalumu za SMZ ,Mhe. Haji Omar Kheri , uliofanyika huko katika ukumbi wa Jamhuri Hall Wete Pemba.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Idara maalumu za SMZ, Mhe.Haji Omar Kheri, akizungumza na Viongozi walioingia katika Ugatuzi wa madaraka mikoani huko katika ukumbi wa Jamhuri Hall Wete-Pemba.
Baadhi ya watenadji wa Jeshi la kujenga Uchumi (JKU) wakitowa huduma katika mabanda yao ya maonesho ya siku ya chakula Duniani huko Chamanangwe Kisiwani Pemba.

Naibu Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar , Hassan Khamis Hafidh, akizungumza na Watendaji wa Jeshi la kujenga Uchumi katika moja ya Mabanda ya maonesho ya siku ya Chakula Duniani huko Chamanangwe Pemba.
Picha na Said Abrahaman - JKU Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.