Habari za Punde

Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani Yafikia Tamati Katika Viwanja Vya Chamanangwe Pemba Wajasiriamali Waomba Kuongezea Siku Mbili za Ziada

 Balozi Seif akiangalia baadhi ya bidhaa zilizoshonwa na Wajasiriamali wa Zanzibar zilizopo katika mabanda ya maonyesho Chamanangwe na kuamua kuwaongezea Siku mbili wanamaonyesho hao.
Msimamizi wa Mradi wa uzalishaji wa Mafuta ya Alizeti Omar Hamad akimueleza Balozi Seif mbinu na mikakati wanayotumia katika ualishaji wa mafuta hayo katika kiwango kinachokubalika sokoni.
 Balozi Seif akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa Maonyesho ya Siku ya Chakula Duniani katika kundi la Wajasiriamali bwana Nassor Abdulla Nassor.
 Balozi Seif akizungumza na Wananchi wa Mikoa Miwili ya Pemba wakati akiyafunga Maonyesho ya Siku ya Kilimo Duniani hapo Chamanangwe na kutoa siku mbili za ziada kuendelea na zoezi hili ili kuwapa fursa wananchi kuendelea kupata taaluma.
 Baadhi ya Viongozi wa Serikali, Manaibu Mawaziri na Makatibu Wakuu wakifuatilia Hotuba ya Mgeni rasmi Balozi Seif wakati akiyafunga Maonyesho ya Siku ya Chakula Duniani.
 Baadhi ya Wananchi wa Mikoa Miwili ya Pemba wakifuatilia Hotuba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani. 
 Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar {ZECO} Hassan Ali Hassan akipokea zawadi baada ya shirika hilo kuibupa mshindi kwa Taasisi za Kibiashara.
Balozi Seif akimkabidhi zawadi Kamanda wa Chuo cha Mafunzo baada ya Taasisi hiyo kuibuka na ushindi wa Nidhamu.
Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.