Habari za Punde

MNEC Mhe. Theresia Mtewele Kusomesha Mtoto wa Kike Kuazia Kidato Cha Kwanza Hadi Chuo Kikuu.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, MNEC Theresia Mtewele akizungumza na wazazi waliojitkeza kwenye mahafali ya shule ya msingi Kipera iliyopo kata ya Nzihi wilaya ya Iringa mkoani Iringa akiwa sambamba na mwenyekiti wa umoja wa vijana Iringa vijijini Makala mapesa katika mahafali hayo
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, MNEC Theresia Mtewele akimkabidhi cheti kwa mwanafunzi Frola Nongele wa shule ya msingi KiperaMjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, MNEC Theresia Mtewele akimkabidhi cheti kwa mwanafunzi Justine Kindole wa shule ya msingi Kipera
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, MNEC Theresia Mtewele akiwa na viongozi mbalimbali wakielekea kukagua miundombinu ya shule ya Kipera

Na.Fredy Mgunda - Iringa.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, MNEC Theresia Mtewele ameahidi kumsomesha mwanafunzi wa kike atakayefaulu vizuri kwenye mtihani wa darasa la saba katika shule ya msingi Kipera.

Kauli hiyo ameitoa hii leo wakati wa mahafali ya darasa la saba ya shule hiyo iliyopo kata ya Nzihi wilaya ya Iringa mkoani Iringa akiwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.

Akizungumza mbele ya wazazi waliojitokeza kwa wingi kuja kushuhudia watoto wao wakihitimu elimu ya msingi MNEC Mtewele alisema kumekuwa na wimbi kubwa la wanafunzi wa kike wakimaliza shule ya msingi wanakimbilia jijini Daresalaam kufanya kazi za ndani kinyume cha sheria ya nchi inayotaka watoto wadogo wasome kwanza.

“Jamani mkoa wetu wa Iringa umekuwa ukitoa wafanyakazi wengi wa ndani kwenda kufanya kazi katika miji mbalimbali hapa Tanzania kitu ambacho kinaniumiza sana kichwa na sikipendi kitokee tena kwa kizazi cha sasa kwa kuwa elimu inatolewa bure hivi sasa na serikali ya awamu ya tano” alisema Mtewele

Ili kutatua tatizo hilo Mtewele aliwaomba wazazi kuhakikisha wanawapeleka shule watoto wao hadi pale ambapo wanaanza kujitegemea kwa kuwa watakuwa tayari wameshaelimika na wanauwezo wa kufanya kazi za kuleta maendeleo kwa kutumia elimu ambayo wanayo.

Mtewele alisema kuwa atajitolea kumsomesha mwanafunzi wa kike kuanzi kidato cha kwanza hadi chuo kikuu ambaye atafaulu vizuri mtuhani wa darasa la saba na kumuwezesha kwenda kidato cha kwanza na hiyo ndio itakuwa chachu ya wanafunzi wengine kufanya vizuri kwenye masomo yao.

“Ukimsomesha mtoto wa kike unakuwa umeokoa familia yote hivyo ni lazima nitoe kipaumbele kwa mwanafunzi wa kike ila siku nyingine nitafanya hivyo kwa mwanafunzi wa kiume lakini naomba niwape moyo wanafunzi wote wakazane kusoma ili kujikwamia na maisha duni” alisema Mtewele

Aidha Mtewele alichangia mifuko arobaini (40) ya saruji kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya majengo ya shule hiyo na kuahidi kuwa ataendelea kuwatafutia wadau mbalimbali wa kusaidia kuiboresha shule hiyo.

Mtewele aliwaomba walimu wa shule ya mpingi Kipera kufundisha wanafunzi kwa vitendo zaidi ili kuwaongezea wanafunzi uelewa katika masomo wanayoyasoma ili wanafunzi wawe wabunifu katika masomo kwa kuwa wanakuwa wanauelewa mpana wa somo husika.

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi kaimu mkuu wa shule Meckzedeck Mkafule alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamotoza upungufu wa nyumba mbili za walimu,uchakavu wa nyumba tano wanazoishi walimu wa shule hiyo .

“Walimu wengi wanaishi katika mazingira magumu kutokana na uchakavu wa nyumba ambazo wanaishi na kusababisha walimu kuwa na msongo wa mawazo kwa kuwa wanaishi katika mazingira magumu na kusababisha kukosa walimu wengine ambao wanahitajika kuhamia katika shule hiyo” alisema Mkafule

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.