Habari za Punde

NAIBU WAZIRIR MASAUNI AZUNGUMZA NA WADAU WA UTALII ZANZIBAR

 Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Hamad Yussuf Masauni amelitaka Jeshi la Polisi kusimamia vyema majukumu yao ili kuweza kudhibiti uingizaji wa dawa za kulevya katika maeneo mbali mbali zikiwamo sehemu za utalii.

Na Miza Kona Maelezo Zanzibar          19/10/2018
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Hamad Yussuf Masauni amelitaka Jeshi la Polisi kusimamia vyema majukumu yao ili kuweza kudhibiti uingizaji wa dawa za kulevya katika maeneo mbali mbali zikiwamo sehemu za utalii.
Hayo ameyasema huko katika Ukumbi wa Wizara ya Habari na Mambo ya Kale wakati alipokuwa akizungumza na wadau wa sekta ya utalii katika kulinda usalama wa watalii nchini.
Alisema kutokana na jeshi la polisi kuwa na wajibu wa kuimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi na wageni wanaoingia nchini hivyo ni vyema wakaongeza kasi katika maeneo ya utalii ili kuona suala la utumiaji, uuzaji pamoja na uingizwaji wa dawa za kulevya nchini linaondoka .
Alisema  katika kulifanikisha suala hilo ni vyema kwa Jeshi hilo kupanga mikakati  imara ya udhibiti vitendo vionvu vinavyotokana na dawa za kulevya lengo ni kuona wanajamii wanaishi katika hali njema za kiafya.
“Suala la ulinzi la raia na mali zao  ni jukumu la msingi Jeshi la Polisi lakini kikatiba kila raia anatakiwa kushiriki katika kuimarisha ulinzi  kila raia ana haki ya kushirikiana katika kutoa taarifa ili kuweza kudhibiti vitendo vya uhalifu pale vinapotokea nchini”, alifahamisha Mhe. Masauni.
Ameeleza kuwa serikali ya Mapinduzi pamoja na Serikali ya Muungano iko makini katika kupambana na kudhibiti vitendo hivyo ni jukumu la jeshi la polisi kuhakikisha kuwa linaimarisha usalama wa nchi kwa raia pamojana wageni waoingia.    
“Tunawaomba wadau wa utalii waendelee na kazi zao wasivunjike moyo  serikali itaendea kuwasaidia kwani seriklai imekuwa ikuiimarisha jeshi la polisi pamoja na kusimamia matumizi ya rasilimali ya wananchi walio wanyonge zinatumika ipasavyo na kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inaimarika vizuri kwani ndio inayochangiapato la Taifa”, alieleza Naibua Waziri huyo.
 Akizungumzia suala la kuongezwa vituo vya polisi Naibu Waziri Masauni alifahamisha kuwa ni vyema jeshi la polisi likashirikiana na vijana wa polisi jamii katika maeneo yao ili kupunguza vitendo viovu katika maeneo ya utalii.
Ameshauri kuwepo na utaratibu wa kuwasajili watembeza watalii na kuwajua ili kuepuka kuwepo kwa wimbi la watembezaji watalii wasio waaminifu ambao hudaiwa kusababisha usumbusu kwa wageni wanapokuwepo kwenye matembezi yao.   
Nae Kaimu Kamishna wa Polisi Salum Mohammed amesema kuwa jeshi lake limekuwa likishirikiana na wananchi katika kupambana vitendo vya uhalifu.
Alisema katika kufanikisha suala la utumiaji, uuzaji na uingizaji wa dawa za kulevya nchini linaondokaJeshi lake limejipanga vyema kwa kufanya doria katika maeneo mbali mbali mjini na vijijini.
Nao wadau hao wameliomba jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi katika maeneo utalii ili kupukana usumbufu uliopo pamoja na kuboreshwa kwa kupatiwa taaluma ili kuweza kwenda sambamba na sekta hiyo.
Aidha wamesema kuwepo kwa watembezaji watalii wasio waaminifu kunasababisha usumbufu kwa wageni wakati wanapokuwa katika safari zao.
Hivyo aliiomba serikali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kupanga mikakati imara ya kuhakikisha wale wote watembeza watalii ambao hawana sifa wanadhibitiwa, huku akielezea haja ya kutolewa kwa elimu zaidi juu ya umuhimu wa kutembeza watalii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.