Habari za Punde

Mkutano wa Kampeni Mdogo Jimbo la Jangombe Chama Cha DP Viwanja Vya Baja Zanzibar

Mgombe Uwakilishi kupitia Chama Cha DP Bi. Bi.Ramla Muhdhari Daud, kushoto akimsikiliza Mwenyekiti wa DP Ndg. Peter akitowa Sera za Chama Chake wakati wa mkutano wa Kampeni ya Kumnadi Mgombea wao kwa Wananchi wa Jimbo la Jangombe katika Viwanja vya mpira vya baja Zanzibar.  
Mwenyekiti wa Chama cha DP Bwana Peter akimwaga sara za Chama chake kwa Wananchi wa Jimbo la Jangombe katika mkutano wao wa kampeni ya kumnadi mgombea wao Bi. Ramla Mudhhari Daud kwa Wananchi katika viwanja vya Baja Zanzibar.
Wananchi wakiwa katika utulivu wakisikiliza Sera za Chama cha DP katika viwanja vya Baja Zanzibar, na Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikihakikisha zoezi hilo la kampeni linakwenda kwa Amani na Usalama bila ya uvunjaji wa Amaan.

Mgombe Uwakilishi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jangombe Zanzibar kupitia Chama cha DP. Bi.Ramla Muhdhari Daud, katikati akiwa na Viongozi wa Chama hicho wakifuatilia Mkutano huo wakati Mwenyekiti wa DP Mhe. Peter akitowa Seara za Chama hicho kwa Wananchi wa jimbo la Jangombe Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.