Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake katika sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius K.Nyerere na Wiki ya Vijana zilizofanyika leo katika Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga, [Picha na Ikulu.] 14/10/2018.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar zinatekeleza kwa vitendo falsafa ya Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere yenye kusisitiza kufanya kazi kwa bidii.
Dk. Shein aliyasema
hayo leo katika shughuli ya kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na wiki ya Vijana
Kitaifa, zilizofanyika katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na kuhudhuriwa na
viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia
Kassim Majaaliwa.
Katika maelezo yake,
Rais Dk. Sheina alisema kuwa falsafa hiyo ndio iliyopelekea Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzaia Dk. John Pombe Magufuli asisitize kwua “Hapa kazi tu” na
kwa upande wake amekuwa akisisitiza kutofanya kazi kwa mazoea.
Alisema kuwa Serikali
zote mbili zimejidhatiti katika kuzisimamia rasilimali ili ziwanufaishe
watanzania wote kwa kuwaletea maendeleo.
Rais Dk. Shein
alieleza kuwa kumeanzishwa mikakati maaluma ya kuendeleza sekta ya viwanda ili
kuongeza fursa za ajira kuwa na matumizi bora ya rasilimali zilizopo na
kuifanya nchi kuwa na uchumi imara kwa kuleta Mapinduzi ya Viwanda.
Aliongeza kuwa
jitihada zinazochukuliwa na Serikali zote mbili katika kukabiliana na vitendo
vya rushwa na uhujumu wa uchumi ni miongoni mwa jitihada za kuendeleza fikra za
Mwalimu.
Alisema kuwa pale
inaposemwa kwamba zinafuatwa falsafa za Mwalimu, inapaswa kuonesha kwa vitendo
kwamba rushwa inachukiwa na watu hawajihusishi na vitendo vya utoaji na
upokeaaji rushwa.
Akieleza jinsi
anavyokumbukwa Baba wa Taifa, Rais Dk. Shein alisema kuwa atakumbukwa kwa
alivyowaunganisha Watanzania kwa kuviongoza na kuvihamasiha vikosi vya ulinzi
na usalama hadi lwa pamoja akaweza kungolewa Nduli Idd Amin baada ya kuivamia
nchi mnamo mwaka 1978.
“Kwa hivyo kila wakati
tunamkubuka Mwalimu tuwe tunazingatia umuhimu wa kutoisaliti nchi yetu....
tuyapende na kuyathamaini mamabo yetu na wala tusiyabeze... marehemu Mzee Abeid
Karume alituhimiza umuhimu wa kupenda vyetu kwa kusema “Kithamini kiulichochako
mpaka usahau cha mwenzako”,alisema Dk. Shein.
Aidha, Rais Dk. Shein
alisema kuwa ana amini kwamba endapo kila Mtanzania ataamua kwa dhati wa moyo
wake kuyaenzi mambo mazuri ya Mwalimu Nyerere, Tanzania itapata maendeleo
makubwa tena kwa haraka sana.
Dk. Shein alisema kwua
dhamira kubwa ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru ni kuendelea kukumbushana misingi na
mambo muhimu kwa maendeleo ya nchi sambamba na kutoa fursa ya kukutana na
kukumbushana nafasi ya Tanzania mbele ya diplomasia ya Kitaifa.
Alisema kuwa amevutiwa
sana na kauli mbiu ya Mbioo za Mwenge ya wmaka huu isemayo’ Elimu ni ufunguo wa
maisha, Wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu” na kusema kuwa kauli mbiu hiyo
inakwenda sambamba na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dira ya
Maendeleo ya Zanzibar zinazotilia mkazo umhimu wa kuipa kipaumbele sekta ya
elimu.
Alisisitiza kuwa kwa
kuzingatia kwua elimu ndio ufunguo wa maisha Serikali zote mbili zimejidhatiti
kuendeleza hatua ya viongozi waasisi wa Taifa hili Hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ya kutoa elimu bila ya ubaguzi
kuanzia ngazi ya msingi hadi Sekondari.
Alsiema kuwa lengo la
Serikali zote mbili ni kujenga uchumi imara
kwa mnasaba huo anaendelea kuwahimiza kuwashirikisha wananchi na washirika
wa maendeleo kuwekeza katika sekta ya elimu.
Dk. Shein alisema kuwa
kauli aliyoitoa Rais Magufuli kwenye kilele cha mbio za mwenge tarehe
14.10.2017 katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar kwamba katika kipindi cha
uogozi wake na wa Rais Dk. Shein watahakikisha mwege wa uhuru unaendelea
kuwepo.
Sambamba na hayo
alieleza kuwa Serikali zote mbili zitazingatia sana na zzimeweka mipango
mipango maalum katika kuimarisha maendeleo ya vijana na kuwashirikisha katika kuzitafutia ufumbuzi
wa changamoto zzinazowakabili na hasa ukosefu wa ajira.
Aliwtaka vijana
wapende kufanya kazi za halali ili
washiriki vyema katika shughuli za ujenzi wa Taifa na wajibu wao kukumbuka kuwa
hatma ya Taifa hili iko mikononi mwao.
Mapema Rais Dk. Shein
alitembelea mabanda ya Maonyesho ya vijana katika viwanja vya Tangamano mjini Tanga na kuona shughui
mbali mbali zinazofnywa na vijana pamoja na kupata maelezo juu ya shughuli hizo
pamoja na sekta nyengine za maendeleo.
Akizungumza katika
hafla hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera. Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama alisema kuwa vija sita waliokimbiza
Mwenge wa uhuru wakiongozwa na Charles Francis Kabeho waliukimbiza kilomita
28,283.8 katika Mikoa 31 na Halmashauri za Wilaya 195 kwa siku 195 kwa kipindi
hicho cha miezi saba.
Alizitaja Halmashauria
64 zimekutwa na kasoro katika utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo
na kusisitiza kwua Serikali imechukua na itaendelea kuchukua hatua stahiki kwa
kila aliyehusika na kasoro hizo kupitia Ogfisi ya Rais TAMISEMI na mamlaka
nyinginezo.
Sambamba ba hayo
Waziri Mhagama alisema kuwa kwa mwaka 2019 uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru
utafanyika Mkoani Songwe wakatui maadhimisho ya Kilele cha mbio za mwenge wa
Uhuru, Kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana Kitaifa
yatafanyika Mkoani Lindi.
Wakimbiza Mwenge wa
Uhuru Kitaifa mwaka 2018 ni Isaa
Mahamoud Abasi kutoka Mkoa wa Kusini Pemba, Dominick Rweyemamu Njunwa kutoka
Mkoa wa Kigoma, Augusta Paul Safari Kutoka Mkoa wa Geita, Riziki Hassan Ali
Kutoka Kusini Unguja, Ipyana Alinuswe Mlilo kutoka Tanga na Charles Francis
Kabeho kutoka Dar-es-Salaa.
Nao viongozi wakuu
waliohudhuria katika hafla hiyo walitoa salamu zao kwa wananchi akiwemo Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, Spika Job Ndugai kwa niaba ya Bunge, Waziri wa Vijana,
Utamaduni Sanaa na Michezo Balozi Ali Karume kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella kwa niaba ya Mkoa wake
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment