Habari za Punde

Tanga Uwasa Yanufaika na Ruzuku ya Zaidi ya Bilioni 1.2



Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia akielezea mipango ya mamlaka hiyo wakati wa ziara ya ugeni kutoka KFW ya nchini Ujerumani kutembelea mradi wa maboresho ya huduma ya maji safi Jijini Tanga
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly  katikati akionyesha kitu ugeni kutoka KFW ya nchini Ujerumani  wakati wa ziara yao ya kutembelea mradi wa maboresho ya huduma ya maji safi Jijini Tanga.kulia ni Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia akifirahia jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maji Mijini kutoka Wizara ya Maji -Dodoma Mhandisi Lydia Joseph kushoto wakati wa ziara hiyo


Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi  akilakiwa na watumishi wa mamlaka hiyo mara baada ya kuwasili eneo la Mowe

Wageni hao wakishuka kwenye eneo la kusafishia maji Mowe Jijini Tanga  wakati wa ziara hiyo

Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ziara hiyo

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imenufaika na ruzuku ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.2 baada ya kutimiza masharti ya mkopo wa zaidi ya shilingi Bilioni 3 toka katika benki ya CRDB ya utekelezaji wa huduma ya Maji safi Jijini Tanga.

Ruzuku hiyo hutolewa na Benki ya watu wa Ujerumani (KFW) kutokana na Mamlaka husika kutimiza vema masharti ya mkopo huo ikiwa pamoja na zoezi zima la marejesho huku likizingatiwa suala la utekelzaji wa mradi uliopewa fedha hizo.

Hayo yalibainishwa  na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa ziara ya ugeni kutoka KFW ya nchini Ujerumani kutembelea mradi wa maboresho ya huduma ya maji safi Jijini Tanga.

Alisema mkopo huo umewasaidia kuongeza uwezo wa usambazaji wa maji hasa katika maeneo yaliyokuwa na mgawo wa maji bila sababu yaliyochangiwa na udogo wa vipenyo vya mabomba yaliyokuwa yanapeleka maji kwenye maeneo hayo.

“Kama nilivyoonyesha kwamba tumeongeza bomba kubwa la nchi 8 kwa ajili ya kuongeza mgawanyo wa maji kwenye eneo la Neema na kwengineko na kuwepo kwa usambazaji mkubwa kwenye maeneo hayo lakini pia tumejenga mtandao wa km 60 kwa kutumia mkopo huo na ruzuku tuliyopewa”Alisema

Aidha alisema hivi sasa wamejipanga kuendelea kudumisha ubora wa huduma zao ili kuhakikisha wananchi wanaowahudumia wanaendelea kupata huduma bora ya maji katika maeneo yao.

Alisema mbali ya ubora wa huduma hizo za maji lengo kuu ni kuhakikisha wanapokuwa wageni wahisani waweza kupata mrejesho na taswira nzuri kwa mamlaka ili waendelee kupata moyo wa kuwasaidia.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maji Mijini kutoka Wizara ya Maji -Dodoma Mhandisi Lydia Joseph alisema fedha hizo zinalenga katika miradi inayojenga inalengo la kutoa uzoefu kwa mamlaka za maji zinazoingizwa kwenye mfumo huo ili
ziweze kupata uzoefu wa kuwekeza badala ya kuishia kutoa huduma pekee.

Alisema mamlaka nyingi zimekuwa na lengo la kutoa huduma ya maji kwa wananchi kwa miundombinu iliyojengwa na serikali tangu zamani hivyo kutokana na ongezeko la watu na mahitaji yao Mamlaka zinatakiwa kupanua huduma zao.

Mhandisi Lydia alisema mbali na huduma pia mamlaka hizo za maji zinatakiwa kuboresha miundombinu ambayo inahitaji uwezeshwaji kutokana na serikali kuwa na mambo mengi ya kufanya hivyo wakati mwengine huelemewa na uwekezaji jambo ambalo limepelekea kushindwa kuendana na
kasi ongezeko la watu.

“Kwa maana hiyo Mamlaka zetu kama zitapata mikopo na zikijenga uaminifu zinaweza kupata miradi kama hiyo na zaidi ya hiyo huku zikijijengea morali kwa mamlaka zenyewe hasa kwenye uwekezaji na Serikali ikatoa sapoti ”Alisema Mhandisi Joseph.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.