Habari za Punde

Utiaji saini Mradi wa Ujenzi wa Maduka ya Michenzani (Shopping Mall)

 Mkurugenzi Muendeshaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ( ZSSF) Sabra Issa Machano na Meneja wa Ujenzi Tawi la Zanzibar Bai  Hao Chen wakisaini hati za Mradi wa Ujenzi, Nyumba, Maduka, Sehemu ya kueegeshea Magari na Sehemu ya kupumzikia Wananchi  Michenzani  Makontena, katika ghafla iliyofanyika Ukumbi wa  ZSSF Kariyakoo Mjini Zanzibar. Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.
 Mkurugenzi Muendeshaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ( ZSSF) Sabra Issa Machano na Meneja wa Ujenzi Tawi la Zanzibar (CRJE) Bai  Hao Chen wakibadilishana hati za Mradi wa Ujenzi  baada ya kusaini hati za Mradi huo . Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.
 Mkurugenzi Muendeshaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ( ZSSF) Sabra Issa Machano na Meneja wa Ujenzi Tawi la Zanzibar (CRJE) Bai  Hao Chen wakionesha kitabu cha ramani za Ujenzi huo. Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar( ZSSF)  Suleiman Rashid Mohammed  akizungumza  katika ghafla ya utiaji saini Mradi wa  Ujenzi, Nyumba, Maduka, Sehemu ya kueegeshea Magari na Sehemu ya kupumzikia Wananchi Michenzani  Makontena Mjini Zanzibar. Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.
Picha ya pamoja Wafanyakazi wa (ZSSF) na Wakandarasi wa Mradi wa Ujenzi, Nyumba, Maduka, Sehemu ya kueegeshea Magari na Sehemu ya kupumzikia Wananchi  Michenzani  Makontena Mjini Zanzibar. Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.

Na Miza Kona Maelezo Zanzibar      04/10/2018
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ( ZSSF) umetiliana saini ya makubaliano na Kampuni ya Uhandishi wa Ujenzi CRJE East Afrika kuhusiana na Mradi wa Ujenzi wa Maduka ya Michenzani (Shopping Mall)  katika eneo la Michenzani Makontena.
Utiaji saini huo umefanyika katika Ukumbi wa ZSSF Kariakoo baina ya Meneja wa kampuni ya CRJE kutoka China, Bai Hao Chen na Mkurugenzi Mwendeeshaji wa ZSSF Sabra Issa Machano.
Akizungumza mara baada ya utiaji saini Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Suleiman Rashid Mohamed amesema mradi wa ujenzi huo ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015/2020 kwa lengo la kuwaleta maendeleo nchini.
Amesema ujenzi huo utaleta faraja kubwa na matumaini kwa jamii kwani utaondosha wasiwasi uliopo hivi sasa ya kuwa eneo hilo limeachwa bila ya kufanyiwa kazi yoyote.
“Leo nina furaha kubwa na furaha yangu ni kuona kuwa ujenzi  tayari unaanza kwani watu walikuwa wanaona hapafanywi kitu sasa tayari  ujenzi unaanza rasmi wananchi watumaini kupata maendeleo”, Alisema Dkt. Suleiman.    
Aliwata wasimamizi wa ujenzi huo kusimamia vyema majukumu yao pamoja na kushirikiana na wakandarasi wa ujenzi huo ili kuweza kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.
Dkt. Suleiman aliahidi kufuatia ujenzi huo ili kuhakikisha wakandarasi hao wanafuata masharti na makubaliano yaliyomo katika mkataba pamoja na kufanyakazi kwa ufanisi.
Nae Mkurugenzi Mwendeshaji  wa mfuko huo amesema Mradi huo unatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa  ambapo matarajio ya mradi ni kuweza kuleta tija na maendeleo kwa jamii kiujumla.
Amefahamisha kuwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar licha ya kuweka pesa za pencheni na kiinua mgongo pia imekuwa ikiwekeza fedha za ziada kwenye miradi ya maendeleo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.
Ameeleza jengo hilo linakuwa  na ghorofa saba 7, ambalo limegawika sehemu tatu, sehemu ya  maduka, ghorora 5 kwa ajili ya ofisi na nyumba za makaazi, sehemu ya mazoezi, ukumbi wa shughuli za kijamii,  Super Market, Sinema na maeneo mawili kwa ajili ya Benki.
 Mradi wa ujenzi huo unafadhiliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF ambao unatarajia kukamilika mwezi wa June 2020 na utagharimu zaidi ya Tsh bilioni 27.9 hadi kukamilika kwake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.