Habari za Punde

Waamuzi wa Ligi Kuu ya Zanzibar Wanolewa Kwa Ajili ya Msimu Mpya wa Ligi 2018/2019.

Jumla ya waamuzi 40 wanatarajia kushiriki kwenye kozi ya utimamu wa mwili (COPA TEST) inayotarajia kufanyika kesho Ijumaa kwa jiili ya mandalizi ya Ligi kuu ya Zanzibar na ligi nyengine zinazondaliwa na ZFA Taifa.

Akizugumza na KIPINDI HICHI Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi Zanzibar Muhsin Ali Kamara amesema zoezi hilo limepelekwa mbele baada ya matatizo ya kiwanja cha Amani.

Amesema mafunzo haya yameanza na  vipimo vya Afya kwa waamuzi wote leo siku ya Alhamisi kabla ya kwenda uwanjani kwa siku ya ijumaa kwa jiili ya mafunzo yenyewe, aidha amesema mafunzo hayo yataendana na semina maalum kwaajili ya mabadiliko ya sheria za mpira wa miguu kwa muda wa siku mbili .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.