Watalii wakiwa kando ya Mto Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,eneo la Kogatende wakishuhudia tukio kubwa la kuhama kwa Makundi Makubwa ya Nyumbu wakivuka mto kutoka Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Kundi la Nyumbu likijiandaa kuvuka Mto Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Nyumbu wakivuka Mto Mara kuingia katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti .
Baadhi ya Watalii wamelazimika kuongeza siku za kukaa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la aina yake ambalo hutokea kila mwaka .
Kundi kubwa la Nyumbu likiwa katika maandalizi ya kuvuka Mto Mara kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Magari yaliyobeba Watalii yakiwa yameegeshwa kando ya Mto Mara kusubiri tukio la kuvuka kwa Makundi ya Nyumbu katika Mto Mara kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mamba wakiwa Mto Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakiwa katika mawindo ya Mnayama Nyumbu wakati akivuka.
Mnyama Pundamlia wakiwa upande wa pili mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,tunaweza sema ni kama wako hapo kwa ajili ya mapokezi ya Nyumbu wanarudi kutoka katika Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya.
Eneo la Mto Mara ambapo Watalii wakingojea tukio la kuvuka kwa Makundi ya Nyumbu.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyopo Mkoani
Mara,imeendelea kuwa maarufu Duniani na kuvutia watalii wengi zaidi kutoka
maeneo mbalimbali ya Dunia kwa ajili ya kujionea tukio la kila mwaka la kuhama
kwa Makundi makubwa ya Nyumbu kutoka Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya na
kuingia Serengeti.
Tukio hili ambalo hutokea kuanzia mwezi Julai na
wageni kulipa jina la “Great Wildebeest
Migration” mwaka huu linatajwa kuvutia watalii wengi zaidi huku wengine
wakilazimika kuongeza siku za kukaa katika Hifadhi ya Serengeti wakingojea
kushuhudia tukio hilo.
Michuzi blog imeshuhudia Msururu wa Magari ya
kubeba watalii yakiwa na wageni kando ya
Mto Mara kusubiri kujionea hali inavyokuwa wakati wanyama hao wakivuka kwa
makundi kutoka upande mmoja wa mo kuingia Hifadhi ya Serengeti.
Eneo
la Mto Mara ambapo Wanyama hawa wamekuwa wakivuka linatajwa kuwa na Vivuko 10
hali inayochangia waongoza watalii kufuata mwenendo wa Nyumbu kwa sababu si
rahisi kufahamu wapi wataelekea kuvuka jambo ambalo hutumia zaidi ya saa 5 hadi
7 kungojea tukio hilo.
Tukio
la misafara ya makundi ya wanyama hao
kuhama na kurudi hubadilika kila
mwaka kutokana na mabadiliko ya
hali ya hewa
na kiwango cha maji katika
mto mara hata hivyo limeendelea
kuwa kivutio kikubwa kwa wageni .
Kivutio kikubwa
katika misafara ya wanyama hao
ambao wamekuwa wakiondoka
nchini kila mwaka
kuanzia mwezi mey na
kurudi kuanzia mwezi
julay ni namna
wanavyovuka mto mara
na jinsi wanavyokabiliana na wanyama wengine ndani
ya mto huo
wakiwemo Mamba.
No comments:
Post a Comment