Habari za Punde

Mchezo wa Kirafiki Maalum wa Kumuaga Mchezaji wa Timu ya Yanga Kufanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar kesho Kati ya Yanga na Malindi.


Na. Mwandishi Wetu Zanzibar.
Timu ya Yanga inatarajia kucheza mechi nyingine maalumu ya kumuaga aliyekuwa nahodha wake, Nadir Haroub Ally Upapa ambaye sasa ni Meneja wa klabu hiyo.

Mechi hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar Jumamosi ya Oktoba 13 mwaka huu saa 10:00 jioni dhidi ya Mabingwa wa zamani wa Zanzibar na Tanzania, Malindi FC.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omary Kaaya amesema msafara wa Yanga utaondoka kesho asubuhi na mchezo huo utakaokuwa mbashara Azam Sports 2 utatumika pia kujiandaa na mechi zijazo za Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.

Naye Nadir Haroub ambaye pia ni nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Zanzibar, (Zanzibar Heroes), amesema ni jambo la heshima kupata mechi hiyo kwenye ardhi ya nyumbani kwao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.