Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Akutana na Magavana wa Jumuiya ya Pwani Nchini Kenya Kwa Mazungumzo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mhe. Dan Kazungu wakati wa mkutano huo akiwatambulisha Magavana hao kwa Rais kabla ya kuaza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Intercontinental Jijini Naitobi Nchini Kenya kuzungumzia Ushirikiano wa pande hizo mbili katika Sekta mbalimbali zikiwemo za Uvuvi na Biashara.na kuondoa changamoto zilizoko. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kaunti ya Pwani Nchini Kenya Mhe.Salim Mvurya,Governor wa Kwale akizungumza wakati wa Mkutano huo wa pamoja na Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, wakizungumzia Ushirikiano na changamoto zinazozikabili pande hizo mbili katika maswali ya Uvuvi na Biashara.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza wakati wa Mkutano huo na Magavana wa Jumuiya ya Kaunti ya Pwani, kuzungumzia changamoto katika maeneo ya pande hizo, na kukuza ushirikiano wa Biashara.mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Intercontinental Jijini Nairobi Kenya.   
Kushoto Ujumbe wa Tanzania na kulia Ujumbe wa Jumuiya ya Kaunti ya Pwani Nchini Kenya wakiwa katika mkutano wa pamoja wa kuzungumzia changamoto zinazozikabili pande hizi mbili, Mkutano huo umeongoza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Intercontinental Jijini Nairobi Kenya.
Mjumbe wa Jumuiya ya Kaunti ya Pwani Nchini Kenya akichangia wakati wa mkutano huo, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Intercontinental Jijini Nairobi Kenya. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.