Habari za Punde

BOYS WAPIGWA FAINI PAMOJA NA KUFUNGIWA KOCHA WAO NA MENEJA WAOChama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kupitia kwa kamati yake ya kuendesha Mashindano ambao ndio wasimamizi na waendeshaji wa Ligi Daraja la Pili Taifa, Daraja la Kwanza Taifa na ligi kuu Soka ya Zanzibar,  leo imetangaza adhabu mbalimbali baada ya kukaa na kujadili matukio mbalimbali yaliokuwa yamejitokeza katika michezo mbalimbali ya Ligi Kuu Zanzibar.

Timu ya Jang'ombe Boys  wamepigwa faini ya Tsh Laki mbili (200,000/=) kwa kosa la kuonesha vitendo vya utovu wa nidhamu kwa Mashabiki wao baada ya kumfanyia vurugu Muamuzi wa Kati Ali Ramadhan Ibada (Kibo) baada ya kumalizika mchezo kati ya KMKM dhidi ya Jan'gombe Boys ulioshia kwa sare ya bao 1-1 uliochezwa kwenye uwanja wa Amaan Jumapili ya Novemba 04, 2018 ambapo faini hiyo inatakiwa kulipwa kabla ya mchezo wao unafuta dhidi ya Malindi utakaochezwa Jumapili Novemba 11, 2018.

Aidha ZFA imempiga faini ya Shilingi Laki moja (100,000/=) na kumpa onyo kali kocha wa Boys Mohamed Ali Salahi (Richkard) kwa kosa la utovu wa nidhamu kwenye mchezo kati ya KMKM dhidi ya Jan'gombe Boys.

Wakati huo huo ZFA imemfungia michezo miwili (kutokaa kwenye benchi) pamoja na kumpa onyo kali Meneja wa timu hiyo Issa Othman Ali kwa kosa utovu wa nidhamu ndani na baada ya mchezo na kupelekea kuathiri utendaji wa Waamuzi na Kamisaa.

Pamoja na hayo pia timu ya Jang'ombe Boys imepewa onyo kali kutokana na tabia zake za utovu wa nidhamu hasa kwa baadhi ya Mashabiki wake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.