Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Sief Ali Iddi Azungumza na Ujumbe Kutoka Nchini Misri.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Ujumbe wa Wafanyabiashara wa Nchini Misri uliopo Zanzibar kwa ziara ya Siku Mbili.
Balozi Seif  Kulia akiwashawishi Wafanyabiashara wa Misri kufikiria wazo a kuanzisha miradi yao Visiwani Zanzibar wakati akibadilishana nao mawazo.
Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Misri ulikutana kwa mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwenye ukumbi wa majengo ya Kasri ya Kifalme Mizingani Forodhani Mjini Zanzibar.
Kiongozi wa Msafara wa Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Misri ambae pia ni Rais wa Shirikisho la Taasisi za Kibiashara Nchini humo Dr. Sharif  El – Gabaly akimueleza Balozi Seif faraja ya ujumbe wake kutokana na mazingira mazuri ya Uwekezaji yaliyopo Zanzibar. 
Balozi Seif Kulia akimpatia zawadi ya baidhaa za Viungo Kiongozi wa Msafara wa Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Misri   Dr. Sharif  El – Gabaly baada ya kumaliza mazungumzo yao wakishuhudiwa kati kati na Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Balozi Amina Salum Ali.
Kiongozi wa Msafara wa Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Misri   Dr. Sharif  El – Gabaly Kulia akimkabidhi zawadi Balozi Seif  ya Bidhaa zinazozalishwa Nchini Misri.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Misri baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyochukuwa takriban saa Moja na Robo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiagana na Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Misri baada ya kumaliza mazungumzo yao.
Balozi Seif  wa Nne kutoka Kushoto waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Misri pamoja na wale wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar imejitolea na kuwa tayari kuendelea kushirikiana na Misri katika kudumisha uhusiano wa muda mrefu uliojikita katika masuala ya Utamaduni unaofanana pamoja na Maendeleo ya Kiuchumi.
Alisema pande hizo mbili bado zina fursa zaidi ya kushikamana katika misingi iliyoachwa na Viongozi waasisi wa Mataifa ya Misri na Tanzania, mshikamano unaohitaji kuelekezwa katika ushirikiano wa Sekta za Kilimo, Elimu, Utalii pamoja na Viwanda.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Ujumbe wa Wafanyabiashara waandamizi kutoka Taasisi mbali mbali za Kibiashara wa Nchini Misri aliokutana nao katika Ukumbi wa Majengo ya Kasri ya Kifalme iliyopo Mizingani Forodhani Mjini Zanzibar.
Alisema Makampuni na Taasisi za Kibiashara za Nchini Misri zina nafasi ya kuangalia fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwa vile Zanzibar binafsi imeshaamua kuimarisha Sekta ya Utalii ikienda sambamba na muelekeo wa Ujenzi wa miundombinu ya Viwanda.
“ Zanzibar na Misri bado zinahitaji kuendelea kushirikiana katika Sekta za Uchumi ili kuimarisha  uhusiano wa pande hizo zinazofanana Kiutamaduni”. Alisisitiza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Balozi Seif alisema hatua hiyo inayoweza kuungwa mkono na Wafanyabiashara hao wa Misri kupitia Taasisi na Makampuni yao imelenga kuimarisha Sekta ya Uchumi kwa kupunguza changamoto inayowakabili Vijana ya ukosefu wa ajira, kundi ambalo ndio nguvu kazi ya Taifa.
Alisema Sekta ya Utalii na Viwanda iwapo Wafanyabaiashara hao wataamua kwa makusudi kusaidia kuongeza nguvu zao za  Uwezeshaji na Taaluma yanaweza kustawisha Pato la Taifa na kuibua fursa nyingi zaidi za ajira.
Mapema Kiongozi wa Msafara wa Ujumbe huo wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Misri ambae pia ni Rais wa Shirikisho la Taasisi za Kibiashara Nchini humo Dr. Sharif  El – Gabaly alisema Zanzibar ni muhimu kwa Misri kutokana na mfanano wa mazingira ya Kiutamaduni ya Wananchi wake.
Dr. Sharif  alisema ziara yao ya siku Mbili Visiwani Zanzibar imewapa faraja kubwa ya kufurahia utajiri wa Bidhaa za Viungo zinazozalishwa na Wakulima wa Zanzibar wenye kuonyesha ukomavu wa kujituma katika masuala ya kazi za ujasiri amali zinazowapatia kipato.
Alisema yapo mambo mengi waliyojifunza katika ziara yao hiyo ambayo imewapa Wafanyabiashara hao wazo la kuwashawishi Wataalamu wa Makampuni na Taasisi zao kuchangamkia fursa za Uwekezaji zilizopo Zanzibar katika Sekta za Utalii na Viwanda.
Katika mazungumzo hao Viongozi wa Ujumbe huo wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Misri wamefikiria wazo la kuanzisha Kituo cha Biashara Zanzibar kitakachoshughulikia uratibu wa Bidhaa zinazozalishwa Nchini Misri kupatikana Visiwani Zanzibar.
Ziara ya Viongozi hao imepata Baraka kwa kusaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kibiashara kati yake na Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.