Habari za Punde

Dk Mabodi kufanya ziara katika Manispaa na Halmashauri za Zanzibar

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR. 

NAIBU katibu Mkuu wa CCM  Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' kesho Novemba 26,mwaka 2018 anatarajia kuanza ziara yake ya kuangalia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020, katika Mabaraza ya Manispaa na Halmashauri za Wilaya zilizopo katika Mikoa Sita ya Zanzibar. 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu huyo kupitia Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar,  inadhibitisha kuwa tayari maandalizi ya ziara hiyo kamilika. 

Lengo la ziara hiyo ni kukagua kwa kina miradi na masuala mbali mbali ya kiutendaji yanayotekelezwa na Mabaraza ya Manispaa pamoja na Halmashauri sambamba na kuibua changamoto zinazowakabili wananchi ili zitafutiwe ufumbuzi na mamlaka husika. 

Ziara hiyo itaanza Novemba 26, mwaka 2018 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja, ambapo mnamo Novemba 27 mwaka huu ziara hiyo itaendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Kati Unguja.

Novemba 28, mwaka 2018 ziara hiyo itafanyika katika Baraza la Manispaa ya Wilaya ya Magharibi 'A' , na kuendelea Novemba 29 mwaka huu katika Baraza la Manispaa ya Wilaya ya Magharib 'B' .

Mnamo Disemba 3 ,mwaka 2018 ziara hiyo itafanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini 'A', ambapo Disemba 4, mwaka huu ziara inaendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini 'B'. 

Disemba 5,mwaka 2018 ziara hiyo inaendelea katika Baraza la Manispaa ya Mjini, na mnamo Disemba 6,mwaka 2018 yanafanyika Majumuisho ya ziara zote za Mikoa ya Unguja katika Ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

Kwa upande wa Mikoa ya Pemba ziara hiyo itaanza Disemba 12,mwaka katika Halmashauri ya Wilaya ya Wete, na kuendelea Disemba 13 katika Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni. 

Disemba 14,mwaka 2018 ziara itafanyika katika Baraza la Manispaa ya Chake Chake, na Disemba 15,mwaka huu ziara hiyo zitahitimishwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkoani.

Majumuisho ya ziara hiyo kwa upande wa Pemba yatafanyika Disemba 16,mwaka 2018 katika Ukumbi wa Makonyo uliopo Wilaya ya Chake Chake Pemba. 

Pamoja na hayo Chama Cha Mapinduzi kinawasisitiza Viongozi, Watendaji na Wananchi wa maeneo mbali mbali yanayofanyika ziara hiyo kutoa ushirikiano kwa lengo la kufikia natarajia ya taasisi za Serikali kuendelea kutoa Huduma bora na rafiki kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.