Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli Ashiriki Katika Misa ya Maadhimisho ya Jubilie ya Miaka 150 ya Uinjilishaji Afya na Elimu Iliyofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waumini mbalimbali wa Kanisa Katoliki, Maaskofu pamoja na Wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi  katika Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu mara baada ya Misa iliyofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.
  Baadhi ya Maaskofu mbalimbali wa Kanisa Katoliki wakiwa wanawasili kwa maandamano katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya Misa takatifu ya Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa pamoja na Spika Mstaafu Anne Makinda wakiwa katika Misa takatifu ya ya Jubilei ya  Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.
 Baadhi ya Maaskofu mbalimbali wa Kanisa Katoliki wakiwa katika Misa Takatifu ya Jubilei ya  Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa kabla ya kuanza kwa Misa takatifu ya Jubilei ya  Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Polycarp Kardinali Pengo wapili kutoka kushoto waliokaa, Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Nairobi John Kardinali Njue wapili kutoka kulia waliokaa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Majimbo mbalimbali ndani  na nje ya nchi mara baada ya Misa ya Maadhimisho ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Nairobi John Kardinal Njue ambaye aliongoza Misa Takatifu ya Jubilei ya  Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Maaskofu wa Kanisa Katoliki mara baada ya Misa ya ya Maadhimisho ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.
PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.