Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Aendelea na Ziara Yake Jimbo la Bumbuli Wilayani Lushoto.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba wakati alipowasili kwenye kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto akiwa  katika ziara ya Mkoa wa Tanga
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto Novemba 1, 2018.  Kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Novemba 1, 2018. Alikuwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto, Novemba 1, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela na wanne kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Mponde wilayani Lushoto wakati alipowasili kijijini hapo kukagua kiwanda cha chai cha mponde na kuzungumza na wananchi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba katika mkutano aliouhutubia kwenye kijiji cha Mponde wilayani Lushoto
Wananchi wakimpungia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati  alipowasili kwenye kijiji cha Mponde wilayani Lushoto kukagua kiwanda cha chai cha Mponde na kuzungumza na wananchi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Bumbuli wilayani Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Novemba 1, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.