Watu tisa wamejeruhiwa katika ajali ya treni iliyotokea asubuhi ya leo tarehe 2 Novemba 2018 maeneo ya Karakata wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Reli nchini, David Mnyambugha , ajali hiyo pia imesababisha kuharibika vibaya kwa mabehewa mawili na kwamba majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Amesema mabehewa hayo hayafai kuendelea na safari hadi yavutwe, na kwamba taarifa kuhusu safari za treni hiyo itatolewa hapo baadae na mamlaka husika ambayo ni Shirika la Reli nchini (TRC).
No comments:
Post a Comment