Habari za Punde

TCCIA LONGIDO SACCOS WAITAKA SERIKALI KUSIMAMIA SUALA LA ELIMU KWA VYAMA VYA USHIRIKA NCHIN

Afisa ushirika wilaya ya Longido Japhet Mambo akisisitiza jambo wakati akiongea na wanachama wa TCCIA Longido Saccos Ltd ambapo kushoto ni Mwenyekiti wa TCCIA wilaya hiyo Abduraman Konje akifuatalia mkutano huo na kulia ni Mshauri kutoka Shirika la Trias Julius Mlambo akifuattilia picha zote na mahmoud ahmad wa globu ya jamii Longido.

Juu na chini ni sehemu ya wanachama wa saccos ya TCCIA wilayani Longido wakiwa katika mkutano wao wa mwaka wakifuatilia vipengele vya Agenda za mkutano huo picha na mahmoud ahamad longido


Meza kuu wakifuatilia mkutano huo kushoto ni makaumu wa mwenyekiti wa saccos hiyo akifuatiwa na mtendaji wa kata ya Namanga akifuatiwa na mwenyekiti wa Longido Saccos Abdulrahman Konje na Afisa Ushirika na mwisho kabisa ni mshauri wa vikundi kutoka shirika la TRIAS Julius Mambo.

Vijana nao walikuwemo kama sehemu ya mkakati wa serikali kuweza kutengeneza uchumi wa kati wa viwanda vijana ndio nguvu kazi ya taifa lolote kufikia malengo kaama walivyokutwa na kamera ya matukio

Wanachama wakisoma taarifa za kikao hicho hatua kwa hatua katika mkutano huo

Mwenyekiti wa mkutano huo David Wiliam na makamu wake Adela Magani wakisikiliza taarifa ya mapato na matumizi ikisomwa

Wanachama hawakuwa nyuma kufuatilia hatua kwa hatua taarifa ya mapato ya chama chao


Wananchama juu na chini wakifuatilia kikao hicho ambapo waliibua mambo mengi ya kuweza kusaidia kukuza chama chao


Na Ahmed Mahmoud Longido
Vyama vya Ushirika nchini vimetakiwa Kutenga muda wa kutoa elimu kwa wananchama wao lengo likiwa kujua faida za vyama hivyo pamoja na kuweka akiba na kukopa ili kuweza kuwafikia wanachama wengi zaidi hapa nchini kukuza vipato vyao sanjari na kujiwekea akiba na hisa.
Akifungua mkutano mkuu wa mwaka na wa pili wa TCCIA Longido Saccos Mwenyekiti wa Tccia wilaya ya Longido Abrahaman Konje ameitaka serikali kutambua suala la elimu ya uwekaji akiba na uwekaji wa amana kwa watanzania suala ambalo wengi wao bado hawana elimu hiyo.
Amesema kuwa Tatizo hilo ndio maana vyama vingi vya ushirika vimekuwa vinaende kwa kusuasua jambo ambalo sio zuri na linaleta ukakasi kwa wanachama katika juhudi zao za kufikia kuwa na vyama vikubwa hapa nchini vitakavyosaidia maendeleo ya nchi na kuongeza vipato.
“Tatizo hapa nchini wanachama wengi hawana uelewa mkubwa wa masuala ya kujiwekea akiba na Amana(HISA) hivyo kujikuta wanashindwa kutofautisha vicoba na saccos kwa kushindwa kujiletea faida na kuendesha familia kwa kujiwekea amana ili kuweza kuweka na kuwasaidia kusomesha watoto wao na kujiendesha maisha”alisisitiza Konje.
Aidha Kwa Upande wake Afisa ushirika wilaya ya Longido Japhet Mambo amewataka wataalamu wenzake kuhakikisha wanatenga muda mwingi kuvifikia vikundi kwa ajili ya kutoa elimu ya vyama vya ushirikia kwani amegundua vyama vingi wanachama vijijini hawana uelewa hivyo sasa ni ndio muafaka sanjari na kuifafanua sheria namba sita ya mwaka 2013 ya vyama vya ushirika.
Amesema kuwa wengi wa wanachama wa vyama vya ushirika wamekuwa wanashindwa kutofautisha vicoba na saccos na faida zake kwa jamii hususani kuweka akiba na amana jambo hilo limechangia kuwepo mapungufu mengi katika vyama vya ushirika hapa nchini.
Awali akisoma taarifa kabla ya kumkaribisha  mgeni rasmi Mwenyekiti wa TCCIA Longido Saccos Ltd Flora Swai amesema kuwa chama hicho kina jumla ya wanachama 147 ambapo kina mtaji wa kiasi cha tsh.14 milion na kuwataka  wanachama wenzake kuhakikisha wanajiwekea hisa ili kuweza kufikia malengo ya chama chao.
Amesema kuwa kuanzia mwakani wataweka utaratibu wa kuwapongeza wanachama watakaofanya vizuri na kuitaka serikali kuwafikia vyama vya ushirika hapa nchini kuweza kutoa elimu ya uwelewa kwa wanachama wa saccos mbali mbali ili ziwe na tija na kuongeza pato la mwananchi na taifa kwa ujumla.
“Nawasihii wanachama wenzangu kujiwekea amana na kupenda kuuliza ili kuweza kujiletea maendeleo ambapo wengi  wamekuwa pindi kunapotolewa wito wavikao wanashindwa kufikia viwe vya serikali ama vya ushirika nawaomba muwe na moyo wa kuitikia wito pindi unaposikia na sio kupuuzia wito”alisisistiza Swai

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.