Habari za Punde

Diamond Platnumz atembelewa kituo cha Afya Chumbuni

Msanii wa kizazi kipya ambae ni mkuu wa Wasafi Group Abdull Nasib( Diamond Platnumz) akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili na Ujumbe wake katika kituo cha Afya cha Chumbuni Zanzibar alipokwenda kutoa msaada kwa ajili ya Kinamama wanaokwenda kujifungua kituoni hapo.
Msanii wa kizazi kipya ambae ni mkuu wa Wasafi Group Abdull Nasiyb( Diamond Platnumz) akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili na Ujumbe wake katika kituo cha Afya cha Chumbuni Zanzibar alipokwenda kutoa msaada kwa ajili ya Kinamama wanaokwenda kujifungua kituoni hapo.
Msanii wa kizazi kipya ambae ni mkuu wa Wasafi Group Abdul Nasib( Diamond Platnumz) akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Juma (Pondeza) wapili kushoto na Wasanii wengine mbalimbali wakipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha Afya Cha Chumbuni Dkt Mohamed Muslim Mohamed alipokwenda kutoa msaada kwa ajili ya Kinamama wanaokwenda kujifungua kituoni hapo.
Baadhi ya wananchi mbalimbali waliofika katika kituo cha Afya cha Chumbuni Zanzibar ili kumuona Abdull Nasiyb (Diamond Platnumz) wakati alipofika kituoni hapo na ujumbe wake kwa ajili ya kutoa msaada wa Vitu mbalimbali kwa ajili ya Kinamama wanaokwenda kujifungua kituoni hapo.
Baadhi ya wananchi mbalimbali waliofika katika kituo cha Afya cha Chumbuni Zanzibar ili kumuona Abdull Nasiyb (Diamond Platnumz) wakati alipofika kituoni hapo na ujumbe wake kwa ajili ya kutoa msaada wa Vitu mbalimbali kwa ajili ya Kinamama wanaokwenda kujifungua kituoni hapo.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Juma (Pondeza)akitoa hotuba ya makaribisho kwa Msanii wa kizazi kipya ambae ni mkuu wa Wasafi Group Abdul Nasib(Diamond Platnumz)kuzungumza na Vijana na Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika kituo cha Afya cha Chumbuni Zanzibar alipokwenda kutoa msaada kwa ajili ya Kinamama wanaokwenda kujifungua kituoni hapo.
Msanii wa kizazi kipya ambae ni mkuu wa Wasafi Group Abdul Nasib( Diamond Platnumz) akizungumza na Vijana na Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika kituo cha Afya cha Chumbuni Zanzibar alipokwenda kutoa msaada kwa ajili ya Kinamama wanaokwenda kujifungua kituoni hapo.
Picha na Yussuf .Simai - Maelezo -Zanzibar.

Na Khadija Khamis – Maelezo  Zanzibar. 
Tamasha la Wasafi linaloongozwa na Msanii  wa Kizazi Kipya  Abdulnasib ( Dimond) linakusudia kutoa msaada wa  mashine ya utrasound  na oxygen katika  Kituo cha Afya cha Chumbuni kwa ajili ya kuwasaidia akinamama Wajawazito na Watoto katika kituo hicho .
Alisema mbali na kusaidia kituo cha afya, pia amedhamiria kuwapa nyenzo vijana wa jimbo hilo zitazowawezesha kubuni miradi ambayo itasaidia kujiajiri wenyewe .
Hayo aliyasema alipofanya ziara katika  Wodi za Wazazi kituo cha Afya Chumbuni ambapo alipata  fursa ya kukutana na wazazi waliojifungua na baadae kuzungumza na Wananchi wa Jimbo hilo waliofika kumlaki Msanii huyo  .
Alisema kazi kubwa inayofanywa na akinamama ya kuzaa na kulea familia inapaswa kuwajali na kuwathaminiwa na kwa wananchi wenye uwezo hawana budi kuwasaidia ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
 Aidha katika kuonyesha kuthamini mama wajawazito alitoa msaada  wa vifaa mbali mbali kwa ajili ya wodi hiyo na kuwataka vijana wa jimbo hilo kubuni miradi ambapo aliahidi kuwaunga mkono ili iweze  kuwasaidia katika kupata ajira badala ya kutegemea ajira kutoka Serikalini .
Awali Daktari Dhamana wa Kitua cha Afya Chumbuni Mohamed Muhsini alieleza kuwa kituo hicho ni kidogo kulingana na idadi ya wagonjwa wanaofika kutibiwa ambapo kwa mwaka wagonjwa wanaofika 38 elfu hufika katika kituo hicho kupatiwa matibabu hivyo ipo haja ya kutanuliwa .
Nae Mbunge wa Chumbuni Salim Ussi Pondeza alifurahishwa na ujio wa kundi la wasafi katika jimbo lake ambao utajenga ari na kuongeza  hamasa kwa vijana kuweza kubuni njia zitakazowasaidia  kujiajiri  
Aliwataka vijana wa jimbo hilo kujituma na kuiga mfano wa msanii huyo ambae amepiga hatua ya mafanikio katika sanaa ya muziki huku wakielewa kwamba  mziki sio uhuni kama baadhi ya watu wanavyofikiria .

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.