Habari za Punde

Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Ashiri Katika Uchimbaji wa Uwekaji wa Mipira ya Maji Safi na Salama.

Na Mwashungi Tahir. Maelezo,Zanzibar.
SHEHA wa Shehiya ya Kwa Mtumwajeni Rajab Ali Ngauchwa  amewashukuru  wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchimbaji wa msingi na kufukia mipira ya maji ili waweze kupata maji safi na salama na kuondosha tatizo sugu lilodumu kwa muda mrefu katika maeneo hayo.
Hayo ameyasema huko Nyerere Shehia ya Kwa Mtumwajeni wakati walipokuwa wameshiriki pamoja na Mwakilishi wa jimbo hilo  kuchimba misingi na kufukia mipira  kwa lengo la kuondokana na tatizo hili na badala yake kupata faraja hapo baadae .
Amesema mashirikiyano ni kitu kinachohimizwa katika kila sehemu , hivyo amefarijika sana na wananchi wake kwa kujitokeza kufanya adhma hiyo na kujua kwamba sasa tatizo hilo litaweza kuwaondokea katika shehiya hiyo.
Aidha alisema tatizo la maji safi na salama kwa muda mrefu katika shehiya hiyo hayapatikani  kisima kipo ambacho kilichimbwa na viongozi waliyopita lakini kilikuwa hakitoi huduma kwa kipindi kirefu sasa.
Hivyo Mwakilishi wa jimbo hilo Rashid Makame Shamsi amewakabidhi mipira hiyo ya maji safi na salama  roll tatu kwa lengo la kulitatua suala hilo ambalo wananchi hao wamefarajika na kumshukuru kiongozi huyo kwani kisima hicho kwa muda mrefu hakitoi huduma.
Nae Mwenyekiti ya kamati ya kisima Mwadini Shaabani Khatibu wa shehiya hiyo amesema wanatoa shukurani zao kwa mwalishi wa jimbo hilo kwa kuwakabidhi  mipira hiyo na wameahidi wataitunza na kuitunza na kushughulikia vizuri kisima hicho .
Pia amewataka wanachi hao kuchangia kwa  kuweka akiba ili pale inapotokea uharibifu wa mashine katika kisima hicho waweze kukidhi haja na vile vile kusaidia umeme ili huduma iweze kuendelea.
“Nawaomba wananchi tuweze kujipanga kwa kuchangia huduma hii ili tuweze kujiwekea akiba pale yakitokea matatizo  tuweze kuyakabili ili huduma iendelee”. Alisema  Mwenyekiti huyo.
Sambamba na hayo mwakilishi wa Jimbo hilo Rashid Makame Shamsi akiwa ni miongoni ya walioshiriki katika uchimbaji huo na  amekabidhi mipira ya maji roll tatu  na vifa a vya mifereji  ambavyo vitu hivyo vyote thamani yake ni million moja na laki mbili.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.