NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso wa kwanza kulia akikagua
mabomba yatakayotoa maji eneo la Kilapula ambayo yatapeleka maji
wilayani Muheza kutoka Pongwe Jijini Tanga wakati wa ziara yake ya
siku mbili mkoani Tanga kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya
maji kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Maji Tanga Uwasa Mhandisi Jofrey
Gerald
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya
ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia wakati wa ziara yake
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikagua moja ya miundombinu ya
maji wilayani Pangani
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipanda juu kuangalia tanki ya
kuhifadhiwa maji eneo la Ngomeni wilayani Muheza ambapo mradi huo
unatoa maji katika eneo la Pongwe Jijini Tanga na kuyapeleka wilayani
humo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza mara baada ya
kufanya ukaguzi huo
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akiteta
jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Maji Tanga Uwasa Mhandisi Jofrey
Gerald wakati wa ziara hiyo.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akiteta
jambo na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa
ziara yake
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiangalia moja ya miradi ya
inayotekelezwa wilayani Pangani Mkoani Tanga wakati wa ziara yake
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa Kata
ya Madanga wilayani Pangani wakati wa ziara yake kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso kulia akisalimia na mmoja wa
wananchi wa wilayani Pangani mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya
kutembelea na kukagua miradi ya maji
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso katika akiwa kwenye picha ya
pamoja mara baada ya kutembelea mradi huo akiwa na Mkuu wa wilaya ya
Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia na wa pili kutoka kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Maji Tanga Uwasa Mhandisi Jofrey Gerald
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemuagiza
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Kitila Mkumbo kumtafutia kazi nyingine
Mhandisi wa maji Wilaya ya Pangani Novath Wilson kutokana na kushindwa
kusimamia ipasavyo miradi ya maji wilayani humo na kupelekea wananchi
kushindwa kupata huduma hiyo muhimu kwa wakati.
Ametoa
agizo hilo wakati akiwa wilayani Pangani ikiwa ni ziara yake ya siku
mbili mkoani Tanga alipotembelea miradi mbalimbali ya maji
inayotekelezwa wilayani humo na kutokuridhishwa nayo kutokana na
utekelezaji wake kuwa chini ya kiwango hatua iliyomlazimu kuzivunja
baadhi ya kamati za usimamizi wa maji ambapo ziara hiyo alianzia
wilayani Muheza
Licha ya mhandisi huyo kutoa sababu
mbalimbali ya baadhi ya miradi kukwama kutoa maji lakini Naibu Waziri
huyo alionyeshwa kutokuridhishwa na majibu hayo kutokana na baadhi ya
maelekezo aliyokuwa akimpa ili kuweza kukabiliana na changamoto juu ya
miradi hiyo.
“Nimekuita marangapi Wizarani ..tena
nikakukutanisha na viongozi wengi labda watakusaidia na kila mara
nakupigia simu lakini bado unaonekana si mtendaji wa kazi sasa
nitamwambia Katibu Mkuu wetu akutafutie kazi sehemu nyingine lakini
sio hapa Pangani”Alisema Aweso.
Aidha alisema ni jambo la
ajabu ikiwa Serikali inapambana kutenga fedha kwa ajili ya kuwakomboa
wananchi na tatizo la maji huku baadhi ya watendaji wa Serikali
wakishindwa kusimamia vema miradi hiyo na kupelekea wananchi kuichukia
Serikali yao.
Awali akijibu hoja za Naibu Waziri juu ya
sababu za mradi huo wa Maji uliotekelezwa kwa zaidi ya shilingi
Milioni 260 Mhandi huyo wa Wilya alisema mradi huo ulimalizika machi
2013 na unamiaka mitano tangu kukamilika kwake.
Mhandisi
huyo alisema mradi huo unaendeshwa na jumuiya ya watumia maji ambayo
iliundwa kwa mujibu wa kishera na ndio inayoendelea kusimamia mradi
huo ambao kunatakriban mita 1500 kuelekea Kijiji cha madanga ambapo
mabomba yake yalionekana kuchakaa.
“Mh:Naibu Waziri mradi
huu unanjia mbili kuelekea Jaira na Madanga lakini kunauchakavu wa
miundombinu ambapo jumuiya iliyopo haikukusanya fedha ili kuweza
kufanya ukarabati na ndio sababu ya eneo hilo kukosa maji muda
wote”Alisema Mhandisi Wilson.
Naibu Waziri huyo
alishangazwa na hitaji la mabomba hayo kwa urefu wa mita hizo 1500
ambayo ni kiasi cha shilingi milioni 3 kwa ajili ya bomba za nchi
mbili huku jumuiya hiyo ikiwa haina hata shilingi kumi jambo
lililomtia wasiwasi Waziri huyo wa mradi huo kufa.
“Mradi
wa shilingi milioni 260 na leo hakuna hata shilingi kumi na leo hakuna
maji maana yake wananchi hawana maji na kila kitu mnatoa majibu ya
hakuna mradi huu unaweza ukafa na wananchi wakakosa maji swala hili
sitolivumilia”Alisema.
Wakati huohuo amemuiagiza Katibu
Mkuu huyo kuhakikisha Mkandarasi wa Kampuni ya Koberg Constraction Ltd
anaetekeleza mradi mkubwa wa maji toka Pongwe Jijini hadi Wilayani
Muheza analipwa fedha kwa wakati ili kumuongezea ufanisi wa kazi zake.
Akizungumzia mradi huo Mhandisi toka Mamlaka ya Majisafi
na usafi wa mazingira(Tanga Uwasa) Salum Hamisi alisema mkandarasi
anasimamia mradi huo wenye thamani ya shilingi Bilioni 2.6 yupo katika
asilimia 50 huku akikabilia na changamoto ya fedha ili kukamilisha
mradi huo kwa wakati.
Mhadisi Hamisi ambae ni msimamizi wa
mradi huo alisema mradi huo unatarajiwa kumalizika mwezi Mei mwakani
ikiwa Wizara itamlipa mkandarasi fedha zake kwa wakati mradi
utakaosukuma maji katika matank matano na kutarajia kupunguza kwa
kiasi kikubwa adha ya maji Wilayani Muheza.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa Maji Tanga Uwasa Mhandisi Jofrey Gerald
alisema ziara ya Naibu Waziri inamanufaa kwa wananchi hasa baada ya
kutembelea baadhi ya miradi na kubaini baadhi ya chanagamoto huku
baadhi ya kamati zikionekana kutofanya vizuri na kuchukuliwa hatua.
No comments:
Post a Comment